Wednesday, January 27, 2016

KUTOKA KWANGU:....Rangi sahihi katika chumba cha wakuu wa familia (MASTER BEDROOM)

Rangi sahihi zitakifanya chumba cha wakuu wa familia kama mahali patakatifu. Kuchagua rangi kwa ajili ya kupaka chumba cha wazazi (master bedroom) ni moja kati ya hatua kubwa unazochukua wewe mwenyenyumba  za kutengeneza  mahali binafsi. Chaguo lako linatakiwa liendane na
muonekano wako kwa jinsi ya mtindo wako wa kupamba. Kwakuwa nyumba kwenye nyumba nyingi za kisasa chumba cha wakuu wa familia ni kikubwa kuliko vyumba vingine, una machaguo mengi na unaweza kuchanganya rangi tofauti kwenye kuta nne za chumba hiki ile kuleta muonekano wa kipekee.

Kama chumba cha wakuu wa familia kimeungana na bafu na sehemu ya kuvalia inakubidi kuweka mpangilio wa rangi kwenye maeneo hayo yote. Hii haimaanisha kuwa rangi ya chumbani na bafuni zinapaswa kufanana, bali inamaanisha zinapaswa kushirikiana. Kuchukua rangi moja kutoka sehemu moja na kuleta mguso wake kwenye sehemu nyingine kutatengeneza chumba cha kuvutia.

Fikiria mandhari unayotaka kuitengeneza chumbani. Wenye nyumba wengi wanataka mandhari tulivu ya rangi nyepesi. Japo hii haimaanisha kwamba rangi za kuwaka au nzito hazina nafasi kwenye chumba chako. Kama unadhani unazipenda rangi hizi (za kuwaka na nzito) basi fanya kuchanganya kuta na zile tulivu na nyepesi badala ya kupaka rangi moja chumba kizima.

Mara baada ya kuamua ni rangi zipi unataka kupaka, kinachofuata ni kufikiria jinsi gani unataka kuzitumia. Kama unataka rangi ya kuwaka kwenye chumba chako fikiria kijani. Je, unaipenda kijani? Kijani kama cha tunda la epo kina nadharia ya kuwaka na tulivu ambapo kijani hiki unaweza kukichanganya na rangi tulivu kama vile krimu nyeupe. 

Vilevile bluu ya mawingu nayo ni tulivu na laini kwa chumba cha kulala. Kuna jamii nyingi za bluu nyepesi kwa ajili ya kuta za chumba cha kulala endapo hutaki ile bluu nzito. Bluu nyepesi zinafanya vizuri zikichanganywa na kahawia endapo nia yako ni kuchanganya nyepesi na nzito. Laa kama unataka kuchanganya nyepesi kwa nyepesi basi nyepesi ya bluu inaendana na nyeupe. Usishange kwanini mawingu yanapendeza! Vilevile bluu na kijani nyepesi zinapendeza zikitumika pamoja.

Kama nyekundu ndio rangi unayopendelea zaidi, unaweza kuitumia kwenye chumba cha kulala, ila kwa tahadhari. Nyekundu inaleta mhemko na ikiwa nyingi inaweza kuchosha mwili. 

Ama chagua nyekundu iliyofifia au paka kwenye ukuta mmoja tu, ule ukuta  wa tendego (ubao wa kichwani wa kitanda) au ule wenye dirisha kubwa , ili mwanga upunguze makali ya rangi. Kuta tatu zilizobakia paka nyepesi ya kati ya zilizoainishwa juu.

Dondoo ya nyekundu inatumika vilevile kwa njano na chungwa. Hata nyeusi inawezekana kwenye chumba chako cha kulala ila kuwa makini kuichanganya na nyeupe na utaratibu ni uleule wa kuipaka kwenye ukuta mmoja tu kama ilivyoainishwa kwenye nyekundu.



Kupata ushauri wa mapambo ya nyumba na bustani tuwasiliane 
0755 200023

No comments:

Post a Comment