Tuesday, January 12, 2016

PICHA:...Ukuta wa Giza Fenicha za Mwanga

Wapenzi, heri ya sikukuu ya mapinduzi. Nimekutana na picha hii nikaona kuna jambo la kujifunza kuhusiana na kuchagua rangi ya kupaka nyumba.
Ukiangalia hiyo bluu ukutani kusema kweli inaleta ukakasi. Si wengi wangethubutu kupaka rangi hii kwenye ukuta wa ndani wa sebuleni. Ila kwenye hii sebule unaweza usiuone huo ukakasi kwa sababu ya ujanja uliotumika. Ili ku neutralize hiyo bluu mwenye sebule ameamua kuweka fenicha na pazia za rangi za mwanga. Na zaidi ya hapo madirisha yanapitisha mwanga mwingi wa jua. Vinginevyo hii bluu ikiwapo kwenye corridor ni giza tupu au kuwasha taa ndani masaa 24. Laa kuna ile old fashioned ya kupaka ukuta rangi 2, kuanzia kati kushuka chini inakuwa hii bluu na juu inakuwa nyeupe.

Cha kujifunza ni kwamba chagua rangi kwa makini ukiwa na picha nzima kichwani kuwa chumba kitaonekanaje. Inawezekana unaanza kupaka rangi ukuta, cha muhimu uwe tayari unafahamu kichwani utakuwa na fenicha, samani na sakafu (kama utaongezea carpet maana rangi inapakwa baada ya sakafu) ya rangi ipi.

Usisahau kunishirikisha ujuzi wako kuhusu maisha ya nyumbani. Ukishea unajisiskia vizuri.

No comments:

Post a Comment