Wednesday, May 10, 2017

Gauni la bega moja wazi lipo

Yako machache sana wahi kwenye rangi hii na dark green. 0755 200023

Sunday, May 7, 2017

Optimals Lotion ni suluhisho kwa wenye ngozi zenye mafuta

 Kuna Optimals white na Optimals seeing is believing.
Optimals white inatumika na mtu wa jinsia na wa umri wowote kwa ngozi ya uso yenye mafuta ili kuondoa mafuta usoni. Seti hii ina bidhaa 4 ambazo ni Cleanser, Face toner, Face day lotion na Face night lotion.

Cleanser ni sabuni maalum ya kusafisha uso ili kuondoa uchafu wote kwenye ngozi ya uso na vishimo vyake. Bei ni 27,000

Face Toner husaidia kusafisha ngozi ya uso kwa kuipa nafasi ya kupokea lotion. Bei ni 27,000.

Face day lotion ni kwa ajili ya kupaka ngozi wakati wa mwanga wa jua iliyojaa mafuta usoni. Bei ni 38,000

Face night lotion ni kwa ajili ya kupaka ngozi wakati wa usiku. Bei ni 38,000

Optimals seeing is believing ni kwa kuondoa weusi kuzunguka macho na vilevile kundoa makunyanzi. Bei ni 29,000

Kwa mahitaji piga 0755 200023

Magauni ya shughuli, ni pamoja na harusi za Kiislam na Kikristo bei 180,000








Friday, May 5, 2017

Sketi na blauzi..aka Omotola Dress bei ni 35,000


Introducing 2 peace (sketi na blauzi). Sketi ni same color top inakuja kwa red, bluu, green na white. Sizes from Medium to XXL. Bei 35,000

Hii Loose Dress ni 23,000

Inakuja kwa rangi ya  njano, nyeupe na nyeusi.

Njia 7 za kupendezesha meza ya chakula

Ndani ya nyumba kuna meza za aina nyingi kama vile meza ya kahawa, meza ya kwenye korido, meza ndogo za pembeni mwa makochi na  pembeni mwa kitanda bila kusahau meza ya kuvalia na pia wapo baadhi wenye meza katikati ya jiko. Kati ya meza hizi zote meza ya chakula ndio ina changamoto kubwa katika kuipendezesha kuliko hizi nyingine. Hii ni kwasababu ya

Gauni nzuri ndefu za nguva

Iko kwenye rangi hii (maroon), bluu na nyeupe kwa size Large, XL na XXL
Bei ni 28,000. Tuko mchikichini, ukitaka unaletewa ulipo hata kwa size tofauti ujaribu. 0755 200023

Thursday, May 4, 2017

Gauni nyeupe za kwenye shughuli zipo

Wakikuambia dress code ni nyeupe usibabaike. Hii niliyovaa ni Medium, zipo pia Large na XL dukani na online. Jumla na rejareja. Bei ni 28,000
 0755 200023

Wednesday, May 3, 2017

Gauni la mtoko lipo.


Gauni hili linafaa kwa ajili ya mtoko wa usiku. Liko kwenye rangi nyekundu na nyeusi Kwenye saizi Medium, Large na XL. Bei ni 38,000. Tupo online na dukani. 0755 200023

Tuesday, May 2, 2017

LOTION YA LOVE NATURE TEA TREE NI KWA AJILI YA WENYE NGOZI ZENYE MAFUTA

Love nature tea tree ni seti ambayo hutumika kwa watu wa jinsia zote. Ni maalum kwa watu wa umri wowote wenye ngozi zenye mafuta.Husaidia kuondoa chunusi na mapele. Seti hii ina bidhaa za aina tatu ambazo ni cleanser toner na lotion.

Cleanser ni sabuni maalum ya kusafishia uso, huondoa uchafu wote kwenye ngozi ya uso ambapo ni pamoja na make up. Ina ujazo wa ml 150 na hupatikana kwa 19,000

Toner husaidia  kusafisha vitundu vya ngozi ya uso na kuifanya kuwa tayari kupokea lotion.. Ina ujazo wa ml 150 na inapatikana kwa 19,000

Lotion hutumika kutibu ngozi iliyoshambuliwa na mapele na chunusi na pia kusaidia kuondoa mafuta usoni, Ujazo wake ni ml 50 na inapatikana kwa 19,000.

Endapo unasumbuliwa na ngozi yenye mafuta bidhaa hizi ni kwa ajili yako. Tuwasiliane kwa 0755 200023 na inawezekana kuletewa au kutumiwa hadi ulipo.

Karibu

Cream za asili zilizochanganywa na pafyum zipo

Cream za asili za Oriflame zilizochanganywa na perfume zipo. Zinanukia vizuri sana.
07 55 200023

Monday, May 1, 2017

Uzoefu wangu wa safari ya kutembelea Saadani National Park


Habarini wapenzi,

Bila shaka wapo wengi wanaotaka kutembelea vivutio nchini mwetu lakini hawajui waanzie wapi au japo hawapati mwongozo kutoka kwa waliokwisha tembelea maeneo hayo.

Hivyo basi nimeamua kuwashirikisha japo kwa uchache juu ya safari yangu ya siku 3 kutembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani.

Kutokana na uwepo wa sikukuu ya mei mosi ambayo ingefanya mapumzikoni ya mwisho wa wiki kuwa marefu, kama kawaida yangu nilifikiria kitu cha kufanya wakati wa mapumziko hayo.

Nikaamua nataka kwenda na kuona ambapo sijawahi kwenda. Kwanza kabisa nilitafuta watu ambao wana organise safari kama hizi. Nilipowapata nikafanikiwa kununua tiketi ambayo ilijumuisha usafiri, malazi, chakula na kiingilio cha mbugani. Nikawa mmoja wa wateja na huku kukiwa pia na wateja wengine ambao wote tulisafiri pamoja. Kumbuka kuwa unaposafiri kwenye kundi ni gharama nafuu kuliko kusafiri mmoja mmoja.

Safari ilianzia Dar, Afrika Sana ambapo waandaaji walifanya kazi nzuri na mipangilio mizuri na tukaanza safari saa kumi juu ya alama. 
Kuna njia mbili za kuweza kufika Saadani, ya Bagamoyo na ya Wami. Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha njia ya Bagamoyo haikufaa hivyo tukapita ya Wami.

Kutoka barabara kuu ile ya lami pale Wami hadi Saadani kwa mwendo wa kasi ni masaa mawili.

Kwenye saa mbili kasoro tukaingia Saadani. Tukakaribishwa vyema kwa chakula cha usiku na malazi. Malazi yanaweza kuwa kwenye lodge, rest house au tents kuendana na hela yako/waandaaji.
Endapo utataka kwenda huna haja ya kubeba shuka kwani taulo na malazi yapo, kwa bafuni utatakiwa kubeba mswaki na dawa ya meno, chanuo na vipodozi vyako tu. Pia wakati wa dinner na tukapewa muongozo kesho yake. 

Tukaambiwa kuwa kwa vile kipindi hiki ni cha mvua (kwa profession yao wanaita low season) wanyama wana kawaida ya kujificha kwahivyo by saa moja asubuh tunatakiwa tuwe tumeshaingia porini ndipo turudi kwenye saa nne kwa ajili ya kifungua kinywa. Hii ya mapema hivi ni ili kuwahi wanyama kabla hawajajificha.

Tukaenda porini tukafanikiwa kuwaona baadhi ya wanyama kama vile twiga, nguruwe pori, ndege mbalimbali na nyumbu. Baada ya hapo tukarejea restaurant ambapo ilikuwa ni wakati wa chai na baada ya chai tukaanza utalii wa beach.
Tafadhali fahamu kuwa hii ni mbuga pekee Afrika ambayo inaunganika na bahari. Kama ni mpenzi wa kuogelea utakapoitembelea kumbuka kubeba swimming costume.
Hakika niliifurahia sana beach kwa michezo mbalimbali pamoja na wenzangu, kuogelea pamoja na kwamba mvua zilikuwa zinaendelea kunyesha.

Baada ya dinner na some drinks na socializing tukaenda kujipumzisha hadi kesho yake ambapo tuliamkia supu ya mbuzi na capati. Kwa misosi waandaaji nisiwe na hiyana walijiaanda vyema sana. Baada ya supu hii na chai tukarudi vyumbani kwenda kupaki kwa ajili ya safari ya kurudi.

Kwenye saa sita mchana tukaanza safari ya kurejea Dar na hapo ukawa ndio mwisho wa safari yangu.

Ndio hivyo wapenzi! Ukiwa na swali kuhusu safari hii au unataka kununua kati ya viwalo kama nilivyovaa unaweza nicheki kwenye 0755 200023. Asante kwa kusoma!

Sunday, April 30, 2017

Blauzi za shifoni na za kiutamaduni zipo

25,000
Top hizi za culture ni free size




22,000

Blauzi za shifoni zenye vifungo mbele hadi kifuani zipo size Medium, Large na XL.

Zinapatikana kwa jumla na rejareja kwako wewe unayetaka kuvaa au wewe unayetaka kwenda kuuza.
0755 200023

Friday, April 28, 2017

Blauzi za shifoni zipo

Top hii ya shifoni ina kitabaa kingine cha ndani (lining) cha shifoni pia. Kwa wadada wanaojipenda kwa ajili ya kuvalia jeans,tight na sketi za kuendea kazini.
Kwa saizi na bei click kwenye vinavyozwa. jumla na rejareja zipo za kutosha
0755 200023

Haya magauni mawili ndiyo yaliyouzika zaidi

Haya magauni mawili ndio best seller so far. Yapo hadi XXL, zawadi sahihi kwa mother's day
0755 200023

Wednesday, April 26, 2017

Gauni hili linafaa kanisani au harusini

Gauni hili naliita ni la mdada wa heshima anayeenda sehemu aheshimike kutokana na muonekano wake. Linafaa kuvaliwa kanisani, harusini na kadhalika. Kitambaa chake ni cha lace iliyojishikilia humohumo. Yaani haina vitambaa viwili. Kulinunua bonyeza kwenye vinavyouzwa. Simu 0755 200023

Gauni fupi la lace. Nguo zote ni chini ya elfu 41. Bonyeza kwenye Vinavyouzwa

Lace mini dress. Rangi zilizopo ni peach na nyeupe. Size 46, 48 na 52. Bei 40,000
0755 200023

Friday, April 21, 2017

Namna ya kuchagua mtindo wa wallpaper

 
Tunaweza kusema kuwa wallpaper ndio habari ya mjini kwa sasa kwa ajili ya kupendezesha vyumbani kwenye nyumba nyingi za kisasa hasa  sebule. Tatizo lililopo ni changamoto ya mtindo upi ndio sahih kutokana na uwepo wa wallpaper za rangi na michoro mingi mno. Hadi zile flati yaani zisizo na mchoro wowote.

Elimika na dondoo hizi za namna mnunuzi anayetaka kupamba kwa

Wednesday, April 5, 2017

Maandalizi ya ukuta kabla ya kubandika wallpaper



Wanasema kila safari moja kubwa inaanza na hatua moja ndogo. Na hata katika swala la kubandika karatasi za kupendezesha kuta zijulikanazo kama wallpaper, hatua ya mwanzo ndio yenye umuhimu mkubwa. Wallpaper hazishiki au kudumu kwenye kuta zenye mafuta, chafu au rangi inayobanduka. Na ndio maana siwezi kuchoka kusisitiza ni kwa kiasi gani ni muhimu kuandaa kuta vyema kwa ajili ya ubandikaji wa wallpaper.

Kwa kuta zilizopakwa rangi zamani
Hizi ni zile kuta za zamani, yaani nyumba ambazo zilishapakwa rangi kitambo na tayari watu wanaishi.
Endapo lengo ni kubandika wallpaper kwenye kuta za aina hii hazitakiwi kuwa na rangi zilizobanduka na wala maeneo yenye vinundunundu, nyufa au vishimo. Endapo maeneno hayo yapo inabidi kuyaondoa kwa kukwangua na kurekebisha kwa kufuata hatua kama zile za uandaaji kuta wakati unapotaka kupaka rangi ila unaishia kwenye hatua ya primer ambayo huwa ni ya mwisho kabla ya kuanza kupaka rangi yenyewe. Kwa maana hiyo panatakiwa pawe nyororo kabisa. Baada ya hapo ukuta wote usafishwe kwa sponji au kitambaa kilicholoa ili kuondoa vumbi. Mara ukuta huu unapokuwa umekauka ndipo ubandikaji wa wallpaper unapoweza kuchukua hatua.

Kwa kuta zenye wallpaper ya zamani
Kuta nyingi ni rahisi kufanyiwa maandalizi kuliko ambazo zilikuwa na wallpaper tayari na unataka kuibandua ili kubandika mpya. Kwanza kabisa ni vyema ufahamu kuwa ni lazima uondoe kwanza ile ya zamani. Mafundi wengi wanaobandika wallpaper wanajua pia jinsi ya kubandua.

Kuta zenye ukungu
Ukungu unaweza kuonekana kwenye kuta kwa rangi ya njano, kijani, kijivu au nyeusi. Kama hali hii ipo kwenye ukuta unaotaka kubandikwa wallpaper paoshe kwanza kwa maji ya moto yenye blichi. Paache pakauke kabisa halafu papake primer kabla ya kubandika wallpaper. Pakishabandikwa wallpaper ukungu hauwezi kuota tena kwani wallpaper zilivyotengenezwa haziruhusu ukungu kuota juu yake.

Kuta mpya
Endapo kuta/nyumba ni mpya na umefikia kwenye hatua ya kupaka primer (kama tulivyosema huko juu katika maandaliza ya kupaka kuta rangi) unachotakiwa ni kuepuka gharama mara mbili za kupaka ukuta rangi ya mwisho halafu wakati huohuo unataka tena kubandika wallpaper juu yake.  Badala yake unachotakiwa ni kuishia kwenye ngazi ya primer tu kwenye ukuta wowote unaotaka kubandika wallpaper halafu badala ya ngazi inafuata ambayo ni ya mwisho yaani kupaka rangi ndipo unabandika wallpaper.

Natumai msomaji wangu umeelewa vizuri kabisa namna ya kuandaa kuta za aina mbalimbali endapo unataka kuzibandika wallpaper. 

Tunazo wallpaper za michoro zaidi ya 100. Wasiliana nasi kwa namba 0755 200023

VITANDA, MEZA YA CHAKULA NA KABATI LA VYOMBO VIPO

Kitanda 6 kwa 6 bei ni 1.3m

Meza ya chakula ya watu 6 bei 1.3m

Kabati la vyombo very classy 1.2m

Kitanda 5 kwa 6 bei ni 1.2m

Mawasiliano kwa biashara tu ni
0755 200023