Thursday, December 31, 2015

PICHA: NYUMBA YA MAMA MCHUNGAJI RWAKATARE YAWEKEWA ALAMA YA X NA KUANDIKWA BOMOA!!

Unaona hiyo canopy ya getini mdau...ngazi mbili...full architectural
Msanifu kweli aliwekea heshima fani yake...hiki ki balcony cha juu kabisa nadhani ni cha umaridadi tu haendi mtu mule ndio maana hata hakina vizuizi. Landscaper na paving zake za rangirangi ndio usipime.

Hii nyumba inayosemekana kuwa ni ya mama Mchungaji Rwakatare ( au ni Lwakatare?) imetia fora mitandaoni leo kuwa inatakiwa kubomolewa. Kuna anayejua sababu ni nini na je, ni ukuta wa fence tu unaobomolewa au ni nyumba nzima?

Kweli ndio maana maandiko yanasema "jipeni moyo kwani ulimwenguni mnayo dhiki..."duuh unaweza kufa huku unatembea, Ee Mungu!



KUTOKA KWANGU:....Jinsi ya Kupamba Jiko kwa Kuongeza Rangi


Huenda uko kwenye mchakato wa kumalizia chumba cha jiko au labda unakifanyia marekebisho. Jiko la rangi moja linapooza, ukiongeza rangi ndipo unajisikia kweli unapika.

Hizi hapa ni njia unazoweza kutumia ili kuongeza rangi jikoni:

Kuweka marumaru za rangi tofauti kwenye eneo dogo la ukutani.

VITU VIZURI.......MARUMARU/TILES ZA SEBULENI





Hey mpenzi,  tile za ukweli zenye maridadi ya ukweli toka India sasa zinapatikana. Kwa bei ya macho kabla hujazigusa unaweza kudhania ni carpet kwa jinsi zilivyo maridadi. 

Kama wewe au mtu unayemjua anahitaji tuwasiliane nikuelekeze uende uchague ukiridhika kuamua kununua nijulishe nikupe namba ya siri ya discount. Karibu sana na hakika hutajutia hela yako. 

Nakupenda ndio maana nakutafutia vitu vizuri. Kwa wanaonijua kwenye personal level na ambao nimeshafanya nao kazi hizi wanajua ni kwa namna gani nilivyo na jicho la accuracy. Kwahivyo ukiona hadi nime recommend kitu/mtu ni kwamba ni cha ukweli na uhakika.


Wednesday, December 30, 2015

HOME DECOR HAPA NA PALE......CARPET UKUTANI, SOFA, MEZA YA KWENYE CORRIDOR

Carpet sio tena kwa ajili ya sakafuni tu. Huyu katundika ukutani kabisa...ubunifu buana...

Kama una corridor pana unaweza kuweka kikabati kama hiki

Kimeza cha kwenye corridor pana. Wengi tumezoea kuviona hotelini, hata nyumbani weka.. maisha ni hayahaya

Hili kochi kilichonifanya nililete hapa ni huu mguu wake wa tairi. Najiuliza halitakimbia kweli hasa hapa kwenye tiles? Ila ni zuri kwa kusogeza kirahisi

Angalau hapa lipo kwenye carpet si rahisi tairi kuhama

Endapo unataka kununua sofa za sectional nakushauri chagua za rangi hii

MIKAKATI 8 YA KUISHI PASAFI 2016

Mara baada ya sikukuu za mwisho wa mwaka kuanza kumalizika na mapambo yake kuanza kuondolewa ni wakati wa kuweka mikakati ya namna ya kuishi mahali pasafi kwa mwaka huu mpya. 

Na sio jambo la kushangaza kuwa wengi wanaweka mikakati ya mwaka mpya kwahivyo bila shaka moja ya hiyo ni kuhusu mahali unapoishi. Hii ni mikakati ya kukuwezesha kusafisha na kutunza mazingira ya nyumbani kwa mwaka 2016. Jitahidi ufanikiwe katika hili.

1. Tenga fungu kwa ajili ya usafi na matunzo ya nyumba. Bila shaka maisha  ni magumu na wengi wanafikiria mbinu mbalimbali za kubana matumizi, na hili halina ubishi hata kwa nyumbani. Pamoja na hayo ni vyema tukumbuke kuwa mazingira safi kwa ubora wa afya zetu ni kipaumbele namba moja. Unaweza kutumia njia mbalimbali za kuwa katika mazingira mazuri ya nyumbani kwa kubana matumizi, na mojawapo ni kufanya mambo kadha wa kadha bila kumuita fundi au nguvukazi ambayo itaongeza gharama. Kwa mfano, wanafamilia wanaweza kushiriki kutunza bustani na maua bila kuhusisha mtunza bustani wa nje. 

Pia unaweza kuweka majani ya kuhifadhi unvevu kwenye bustani yako ya maua na kukufanya uwe na matumizi kidogo ya kumwagilia. Kwa upande wa kusafisha kama vile vyombo, kutumia maji ya uvuguvugu kutapunguza matumizi makubwa ya sabuni kwahivyo unakuwa umeshabana matumizi. Tumia sabuni za kusafishia ambazo zina matumizi zaidi ya moja na tunza vizuri vifaa vya usafi.

2. Jifunze kusafisha haraka zaidi. Ni watu wachache dunia hii ambao wanapenda kutumia muda mwingi kusafisha nyumba zao. Kwa wengi wetu ambao tuna majukumu mengi ambayo ni lazima tuyakamilishe kwa siku, kujifunza kusafisha haraka haraka ni mkakati mzuri. Ili ufanikiwe katika kusafisha kwa haraka hakikisha unahifadhi vifaa vyako vya usafi eneo moja. Haifai unataka kudeki huku unaanza kutafuta dekio na kukasirika hulioni kiasi kwamba hata ari ya usafi inaondoka. Pia anza na eneo ambalo sio chafu sana na usipoteze muda kusafisha sehemu ambayo sio chafu. Kwa mfano umesafisha jokofu wiki iliyopita basi wiki hii usihangaike kusafisha tena. Kuepuka kurudia rudia safisha kuanzia juu kushuka chini.

3. Epuka mrundikano. Nyumba iliyovurugwa inahitaji kitu zaidi ya usafi. Kuwa na mkakati wa kupunguza vitu ndani ya nyumba yako ili kuepuka  mrundikano. Kuondoa mrundikano ni njia kuu ya kukufanya uweze kusafisha kwa haraka bila kupoteza muda. Nyumba isiyokuwa na mrundikano ni rahisi kusafisha kuliko ya kinyume chake.

4. Kuwa na mpangilio. Mara mrundikano unapoondioka, hatua nyingine kubwa inayofuata ni kupanga vizuri vitu vilivyobakia. Mara kila kitu kinapokuwa na makao yake ndani ya nyumba yako mrundikano unakuwa sio hoja tena na kusafisha kunarahisishwa.

5. Andaa ratiba ya kusafisha. Kila dakika kuna kitu cha kusafisha, lakini huwezi kusafisha kila dakika. Kuwa na ratiba ya usafi kunawezesha urahisi wa kusafisha kwa siku, kwa juma na kwa mwezi. Ratiba ya kusafisha ina faida ya kuu kuwa hupotezi muda wako kusafisha vitu ambavyo haviko kwenye ratiba ya kusafisha siku hiyo.

6. Hamasika zaidi kusafisha. Kuna wakati hamasa ndio kitu kinakosekana kwenye utunzaji wa nyumba zetu. Sio rahisi kila wakati kuhamasika kusafisha, lakini kuna vitu rahisi ambavyo vinaweza kukuhamasisha. Hamasa ya kusafisha inafanya usafi uende haraka. Tafuta hamasa inayokufanya usafishe, labda unataka upige picha baada ya kusafisha au unataka uache nyumba safi au unapenda ugeni wa mara kwa mara, au ni kujaribu sabuni mpya ya kusafishia au ni kupanga upya chumbani na kadhalika.

7. Shirikisha wana familia wote kwenye kusafisha. Kugawa majukumu ya kusafisha hata kwa wale wanafamilia wadogo kabisa ni mkakati mzuri wa kufanya mazingira ya nyumbani yawe masafi. Mtu anaposafisha anaelewa ugumu wake kwahivyo hata kuchafua anapata ukakasi. Na kwa wale wanaoweza kusafisha vizuri wanasaidia zoezi zima limalizike kwa uzuri na haraka.

8. Nyumba safi ni pamoja na kufanya ukarabati. Hakikisha pale panapohitaji ukarabati panarekebishwa mapema iwezekanavyo.


Na wewe msomaji wangu nishirikishe mikakati unayotumia kuhakikisha unaishi mahali pasafi. Nijulishe kwa simu/whatsapp 0755 200023

Tuesday, December 29, 2015

BARBEQUE (CHOMA CHOMA) NI NJIA RAHISI KULIKO ZOTE YA KUANDAA SHEREHE NYUMBANI

Haijalishi kama hutakubaliana na mimi ila nakuhakikishia kuwa choma choma ndio njia ya gharama nafuu na ya haraka na isiyo na mlolongo mrefu kama una kijimnuso nyumbani. Na kama tujuavyo sherehe za nyumbani sio za umati.

Sababu hizi hapa:

1. Maandalizi ni mafupi sana. Yaani tuseme unachoma kuku, ni kiasi cha kuweka nyama zako viungo, kusubiri kwa muda na kuanza kuchoma.

2. Unaweza kuchoma wewe mwenyewe na hapa ndio penye bana matumizi kwani huhitaji mambo ya caterer.

3. Unaweza kuchomea popote nje ya nyumba. Hata kwenye garden upande wa majani kwakuwa jiko la kuchomea halidondoshi moto au majivu ya moto chini useme yataunguza majani na maua.

4. Nyama choma zinaendana na ndizi za kukaanga (za kuchoma zina usumbufu) na kachumbari, ambapo wewe na familia yako mnaandaa tu fasta.

5. Rasilimali zinazotumika, kwa mfano mkaa ni kidogo sana

Kama huwa unapenda kuburudisha nyumbani niambie njia rahisi unayotumia ili tujifunze kutoka kwako pia. Simu/Whatsapp 0755 200023

HOUSEKEEPING....Profesa Jay akifanya usafi


Nimeguswa na hii picha ya Mhe. Joseph Haule aka Profesa Jay akifanya usafi..wanaume mkiamua mnaweza. Safi sana Prof 


SIO LAZIMA UMUITE FUNDI:.....Jinsi unavyoweza kubadilisha rangi ya carpet

Hili ni carpet lako lililo plain

Bandika tape kwa ajili ya kutengeneza patterns kama hutaki libaki na rangi moja. Bila shaka ulishawahi kumuona fundi rangi akiweka tape hivi.

Tape zimeshamiri kila mahali na ina maana likishapakwa rangi litabaki na pattern hivi

Taaatiibu unaanza kupaka rangi unayotaka, huyu kachagua yellow

Tape zimeondolewa na carpet kamilifu hili hapa

Unaliweka zako kwenye varanda na fenicha juu yake linakuwa limetulia hivi.

Na wewe nitumie picha ya project yoyote unayofanya hapo nyumbani kwako
photo credit: todayshome

HOME DECOR HAPA NA PALE...PIPI, MAUA, FERN

Nimeguswa na huu ubunifu wa kugandishia pipi kwanye mpira namna hii. Imagine pipi zenyewe si ghali hata wewe unaweza kufanya pale unapoamua ku entertain nyumbani tuseme ni kwenye birthday ya mtoto kwa mfano, kwa ajili watoto wanapenda pipi. Utakapofanya hivyo nitumie picha

Haya maua mazurije yanafanana na pipi

Huyu mchoraji anastahili pongezi, kaamua ku deal na shape mbalimbali za jani la fern


THEY HAVE MY TRUST......Vitanda vya Chuma vya Deka

Habari rafiki yangu. "They Have my Trust" ni bidhaa na huduma za home decorations ambazo nimezipitia na kuziamini na kwahivyo nikiku refer wewe mteja ni kwamba ni kitu nina uhakika nacho, na kwa vile unaniamini ni kwamba na hizi bidhaa utaziamini. Mtengenezaji wa vitanda kama hivi na fenicha nyingine nyingi za chuma ni Janeth Kambona simu 0715 767 006, Kinondoni Dar. Endapo utataka kununua au kutengenezewa fenicha yoyote toka kwake nijulishe nikupe code yangu ya punguzo la bei. Welcome..




Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani ambayo unataka Watanzania waijue? Nijulishe simu/whatsapp 0755200023


Friday, December 18, 2015

PICHA: HIVI UZUNGUNI KWANINI HAWAOKOTAGI KWENYE BUSTANI

Hii picha nzuri mpya ni rasmi iliyotoka ya familia ya mwana mfalme wa Uingereza kwa ajili ya kutoa heri ya sikukuu. Ila mazingira ya hii picha kama unavyoyaoona bustani imedondokewa na majani mengi makavu na hayajaondolewa. 

Na ni mara nyingi naona picha za hivi za bustani huko ughaibuni. Huwa najiuliza kwanini hawasafishi hizi bustani kwa kuondoa haya majani makavu? Wenye exposure zenu hebu semeni neno why inakuwa hivi?..

Thursday, December 17, 2015

UKIKUTANA NA VINYAGO HIVI VIKIUZWA BEI CHEE JE UTAVINUNUA?

Sometimes hatutakiwi kuyafanya maisha serious sana. Sema ukweli, je ukikutana na kinyago kama hiki utakinunua? 


CHRISTMAS DECOR HAPA NA PALE

Picha yangu na wishes za sikukuu kutoka kwa shabiki!
Wazungu wana mambo..ukishindwa kutundika ukutani unamvalisha hata jibwa


Kadri miaka inavyoenda miti ya krismasi inakuja kwa rangi na mitindo mbalimbali lakini ile frame/umbo lake ya msing liko palepale



Na wewe rafiki nirushie picha ulivyopamba kwa ajili ya sikukuu ili tuburudike na kujifunza kutoka kwako pia.

Wednesday, December 16, 2015

ZINGATIA HAYA PAZIA ZAKO ZIVUTIE

Kuwa na pazia zinazovutia inaweza kuwa changamoto.Kuna mambo mengi unayopaswa kuzingatia kuhakikisha kwamba pazia husika zinaoana na rangi na mapambo ya chumba chako na mpangilio wake. Baadhi ya mambo hayo ni haya yafuatayo:

·       Kwanza kabisa weka pembeni suala la muonekano kwani lengo namba moja la pazia ni kufunika dirisha. Kwa sehemu kubwa lengo hili ndilo litakubana kwa njia nzuri unapochagua pazia zako. Kama unataka pazia zinazoleta faragha au giza kabisa, unatakiwa kuwa na pazia zenye kitambaa cha pili (lining) kwa ndani. Kitambaa hiki kitaongeza gharama lakina kina faida nyingi kama vile: kuzuia kile kitambaa cha nje cha pazia (ambacho ndio maridadi) kisiharibiwe na jua na hivyo kudumu muda mrefu. Kitambaa cha ndani pia kinaongeza uzito wa pazia na hivyo kulifanya limwagike vizuri na kutulia bila kuhamahama hata kama umewasha pangaboi. Na vilevile lining linafanya pazia kuonekana la kifahari. Pazia za hivi nyingi ni za kushonesha, huzikuti zikiwa zimeshonwa tayari.

NJIA ZA KUPAMBA SIKUKUU HII


Chochea furaha na msisimko wa kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kupamba ndani na nje ya nyumba yako. Vitu rahisi hata  kama ni vijipambo vya meza tu huleta tofauti kubwa ya muonekano wa mazingira ya nyumbani.
Baadhi ya njia tofauti unazoweza

Friday, December 11, 2015

NAFASI YA KAZI.....SALES OFFICER AT CLEOPATRA FURNITURE

Tanzania At Hoom Company Limited “CLEOPATRA FURNITURE MART” has more than fifteen years experience in making furniture. In Tanzania we are providing services for more than three years. This experience is derived from the professional Egyptian arts. We are looking for people who care about the quality products and services they represent to their customers and co-workers.

1.      Job Title: Sales officer
2.      Report to: Sales Co-coordinator
3.      Location: Nyerere road plot 94, opposite diamond motors Kiwalani industrial Dar-es-salaam.
4.      Purpose: To work within departmental sales and operational plans to maximize revenue. To deal         with all sales enquiries from initial contact to full delivery of the service and after sales customer care

KEY DUTIES AND RESPONSIBILITIES FOR THE POSITION
1.      Greeting guests upon arriving in our retail showroom and learning their motivation for their visit; really getting to know them and developing long – term relationships
2.      Presenting and discussing various home furnishings product options based upon your discovery of the prospective clients lifestyle, needs and goal
3.      Marketing new sales and specials events
4.      Assisting customers in financing, purchasing, delivery and ultimate satisfaction
5.      Increasing personal knowledge of products, sales techniques and promotions thought continuous professional training and development.
6.      To deal with all customer enquiries in a professional manner and within set guideline, demonstration sound knowledge of all aspect of the products on offer.
7.      To assist the sales Co-ordination to seek and build ongoing relationships with clients in order to sell  service in line with the departmental sales and marketing operational plan and budget targets.
8.      To ensure that each stage of sales is completed in a time and accurate manner, include: preparation of quotations, confirmation of requirement , issuing of contracts and invoices, service delivery

REQUIRED QUALIFICATIONS AND EXPERIENCE
·        Experience in high customer expectation
·        Entrepreneurial and team oriented
·        Coachable and self directed person who is always willing to learn
·        High energy people person relentless in pleasing the customer
·        Basic computer knowledge is required
·        Strong interpersonal and communication skills; a great listener
·        High school or diploma in sales is required

HOW TO APPLY
If you believe you are the ideal person we are looking for submit your application letter and curriculum vitae detailing your experience with three referees to
EMAIL : cliopatra.furniture@gmail.com , hosamkassem@gmail.com
Or hand delivery: Nyerere road plot 94 (SIDO BUS STAND) Opposite Diamond Motors Kiwalani industrial area - Dar-es-salaam - P.O.BOX:72540 DAR ES SALAAM

Deadline Dec31, 2015

Wednesday, December 9, 2015

ZIJUE RANGI MPYA ZA CHENGACHENGA ZA KUPAKA NYUMBA








Rangi za ukuta za chengachenga zipo kwenye chati kwa sasa, usishangae kwani ni wataalam wa rangi wanazidi kufanya yao technology inakua kila leo. 

Rangi hizi  zinapatikana Crown Paints Tazara Dar. Endapo utafika pale kununua nijulishe kwanza kwa simu/whatsapp 0755 200023 ili nikupe namba ya siri upewe discount kwa jina langu. 

Tuesday, December 8, 2015

NAMNA RAHISI YA KUANDAA SHEREHE NYUMBANI MSIMU HUU WA SIKUKUU


Kama tujuavyo sikukuu za mwisho wa mwaka zimekaribia. Na sikukuu maana yake ni sherehe na shamrashamra kwa wingi. Hivyo basi kwa lengo la makala hii nimefanya mahojiano na Asna Mshana ambaye ni mtaalam wa kuandaa sherehe na anaelezea ni kwa njia gani rahisi kabisa unaweza kuandaa sherehe yako nyumbani msimu huu wa sikukuu. Twende pamoja tuelimike na dondoo hizi za kuandaa sherehe ndogo ya sikukuu nyumbani bila kutoa jasho.

·Kwanza kabisa unapaswa kujiuliza ni