Tuesday, July 31, 2012

Kazi yangu leo

So baada ya kushauriana na mteja wangu tulikubaliana kumshonea nguo mshono huu. Hiki kitambaa ni material toka Somalia, nguo ina lining na shingo yake ni assymetrical kama unavyoiona zipper iko ubavuni.

Monday, July 30, 2012

Simple & Chic


Gauni hili la rangi ya tangarine ni kutoka spring/summer collection ya Victoria Beckham ya 2012. Remember tangarine is the color of the year. Do you think you will look the best in this?

Sunday, July 29, 2012

African Attire Sunday

Je unapenda mtoto wako mdogo aulambe Kiafrika? Call me 0755 2000 23

Saturday, July 28, 2012

Friday, July 27, 2012

My Article for Newspaper: Jinsi ya kutoka bomba na nyekundu


Jinsi ya mwanamke kuonekana bomba na gauni jekundu

Nyimbo zimeimbwa, sinema zimechezwa na maonyesho ya mavazi yamefanyika yote ni juu ya gauni jekundu. Gauni jekundu moja kwa moja linakufanya uchomoze nje ya jopo kwa hivyo kujiamini ni kitu kinachotakiwa wakati umelivaa. Nyekundu ni rangi ya mahaba. Mfikirie mdada ndani ya nguo nyekundu ambaye anafanya shingo ya kila mwanaume mwenye damu nyekundu imgeukie.

Nyekundu ni rangi moja ambayo wanawake wachache wanathubutu kuvaa. Nyekundu ni rangi inayoambatana na mapenzi, na mategemeo ya uhai.

Mwanamke anayevaa nyekundu sahihi anaonekana bomba kwa kila amtazamaye. Nyekundu hiyo ni ile inayoendana na umbo lake na rangi ya ngozi pia.

Angalia, kuna nyekundu za kuwaka na zilizopoa.
Baadhi ya vitu vya kuzingatia kabla ya kuthubutu kuvaa gauni lako jekundu la mahaba, ambalo unatamani mara kwa mara kulivaa ni hivi:
  • Angalia ni muda gani wa siku unapovaa rangi nyekundu. Wakati wa mchana chagua nyekundu kama rangi kuu lakini kuwe na rangi nyingine ndogo. Kama unavaa gauni jekundu usiku vaa nyekundu tupu kwa ajili inaonyesha mahaba zaidi.
  • Nyekundu zilizopoa zinapendeza kwa ngozi mng’avu, chagua nyekundu kuendana na rangi ya ngozi yako. Vaa nyekundu za kuwaka kama rangi ya ngozi yako ni nyeusi.
  • Kama wewe ni mwanamke mwenye mwili mdogo vaa nyekundu za kuwaka na za kushika mwili. Hii itakufanya uonekane kwa ajili mwili wako ni mdogo. Unaweza pia kuvaa zenye michoro ili kuleta mvuto kwa mtazamaji. Chagua nyekundu yenye michoro kwenye kiuno au vaa mkanda wa rangi za pundamilia au chuichui ili kuelekeza macho ya mtazamaji kwenye nyonga.
  • Kwa wanawake wenye maumbo makubwa, vaa nyekundu zilizopoa kama ya damu ya mzee au nyekundu ya mvinyo mwekundu ili kuondoa macho ya mtazamaji kwenye mwili wako. Pia waweza chagua nyekundu yenye michoro kuanzia kwenye makalio shuka chini ili kufanya macho ya mtazamaji yasielekee kwenye tumbo lako kubwa.
Jijue.
Unapendeza kwenye nyeusi au bluu ya kuelekea weusi au kijivu? Kama ndio basi utapendeza kwenye nyekundu zilizopoa. Kata tikitimaji na uangalie ile nyekundu iliyopo ndani yake. Hii nyekundu ya tikitimaji ni ile iliyopoa ambayo itakupendeza wewe. Chagua nyekundu za aina hii.

Kama unapendeza kwenye rangi ya chugwa kuliko kwenye nyeusi ina maana utaonekana bomba kwenye nyekundu ya kuwaka. Angalia nyanya iliyoiva. Hii ni nyekudu ambayo itakufaa sana wewe.  

Mara unapojua nyekundu yako basi anza kujijengea kabati la nguo la nyekundu.
Sasa tayari una nyekundu zako, chagua rangi nyingine chache ambazo zitaendana na nyekundu na rangi yako ya ngozi. Zangi za wanyama kama chuichui na pundamilia zinaendana vyema na nyekundu.
Vitupio vya kuvaan na gauni jekundu
Gauni jekundu halihitaji vitupio kwa sana kwa ajili tayari nyekundu ina mvuto. Uwe makini unapotupia na gauni jekundu kwani ukiremba sana utakuwa kama mdoli. Vaa gauni jekundu na urembo wa dhahabu au silva. Usivae vyote kwa pamoja. Unaweza kutupia kimkufu na bangili pia paka rangi ya kucha na mdomo inayoendana na nyekundu ya nguo yako. Tena kama ukitupia na mkanda mweusi itakuwa bomba zaidi.
Zaidi ya viatu vyeusi gauni jekundu waweza pia kuvaa na viatu vya rangi ya silva.
Nyekundu imejaaliwa, ni rangi inayoleta mvuto. Si rangi ya mtu anayetaka kujificha kwenye jopo. Lakini kama unataka kuwa nyota, kama umechoka kufuata mkumbo, kama unatk kuwa tofauti basi nyekundu ni rangi ya kuvaa.

Makala hii imeandaliwa na Vivi O.Machange 0755 200023