Wednesday, April 8, 2015

House Tour: TUJIFUNZE CHOCHOTE TOKA NYUMBA HII YA CAMILLA..

As lengo kuu la blog hii ni kuongelea zaidi kuhusu nyumba, nimependa tuangalie sehemu mbalimbali za nyumba hii ya mtandaoni ya Camilla ambapo naamini "in near future" nitapata wabongo watakaonipa ushirikiano wa wao pia kuelezea sehemu mbalimbali za nyumba zao..Ukimaliza kusoma hii post utakuwa umefaidika na mawazo mawili matatu yatakayorahisisha maisha hapo nyumbani kwako
 Angalia jinsi Camilla alivyopamba sehemu hii ya kuingilia unapotokea nje. Hiyo doormat naamini mlango utakuwa unafunguka kwa nje. Halafu angalia na hiyo decorative mirro ukutani.

 Mume wa Camilla ni mutu ya shule..kwahivyo kwake ameweka library. sio kila mtu ana library nyumbani na hata kama ipo inakuwa ni kishelfu tu cha kishkaji sio kubwa hivi..
 Ili kuondoa mrundikano Camilla ameweka vikapu kila mahali kwa ajili ya kuhifadhia. Kwa mfano unaona hapo juu ya coffee tabke kaweka kikapu. Hii ni kwa ajili yeye ana watoto wanne wadogo.
 Usiogope kumwachia mtoto wako mdogo acheze sebuleni..inachotakiwa tu ni kuwa na kikapu cha kuhifadhi vitoi vyake ili asivitupe kila mahali.
 Muonekano wa sebule na dining ya Camilla. Yeye kaweka carpet la kutupia sebuleni tu, hajaweka la wall to wall.
 Jikoni kaweka kimeza hiki kati kwa mlo wa fasta
 Huo mlango ulio wazi ni stoo iliyounganika na jiko, Pia kaning'iniza ubao wa kuandika ratiba ya msosi. Hata kama wewe huweki ubao kama huu lakini ni vyema kuwa na ratiba ya chakula jikoni.
 Camilla hapendi kabisa mrundikano..angalia jiko lilivyopangwa...kitchen counter haijajazana vifaa.
 Kuwa na sehemu nyingi za kuhifadhia inasaidia sana kusiwe na mrundikano. Ona alivyo na droo nyingi jikoni. Pia hizo handle za droo zinavutia na bila shaka ni imara.
 Sinki la bafuni kwa watoto lipo nje kidogo ya choo. Na hapo kaweka kile cha kukanyagia ili mtoto mdogo afikie sinki aweze kupiga mswaki vizuri. Hivyo vidude ya watoto kukanyagia chini ya sinki hata bongo vipo.
 Hiki chumba yeye amekitengeneza kwa ajili ya vitu vya watoto wanavyotumia kila siku, kwa mfano viatu vichafu ambavyo watavyaa tena kesho yake nk
 Chumba cha watoto cha kuchezea, ambapo makorokoro yao yote ya kuchezea wakiwa ndani ya nyumba yako humu
Chumba cha mtoto mmojawapo cha kulala. Kitanda ni cha chuma na kadri mtoto anavyokuwa atakibadilisha.
Umevutiwa? Ungependa kunishirikisha sehemu yoyote ya kwenye makazi yako. Hata kama ni zulia ulilonunua ukaweka kwenye chumba chako kikapendeza na ungependa ku share...tafadhali nijulishe.

No comments:

Post a Comment