Tunaweza kusema
kuwa wallpaper ndio habari ya mjini kwa sasa kwa ajili ya kupendezesha vyumbani
kwenye nyumba nyingi za kisasa hasa sebule. Tatizo lililopo ni changamoto ya
mtindo upi ndio sahih kutokana na
uwepo wa wallpaper za rangi na michoro mingi mno. Hadi zile flati yaani zisizo
na mchoro wowote.
Elimika na dondoo
hizi za namna mnunuzi anayetaka kupamba kwa
pambo hili anavyoweza kununua ya
mtindo sahihi kwa chumba sahihi.
Unapotaka kupamba kwa wallpaper kuna
maswali kadhaa ya mitindo ya wallpaper unatakiwa uweze kujijibu. Je
chaguo zuri kwako ni wallpaper yenye michoro au iliyo flati? Jibu hapa
linategemea na ladha binafsi ya mwenye kutaka kupamba. Wallpaper yenye michoro
hata kama ni ya rangi sawa na ya wallpaper yenyewe, kwa kawaida inasaidia
kuficha makosa yoyote yaliyopo ukutani.
Wallpaper flati inakupa wigo mpana
wa muonekano wa kung’aa na metaliki. Lakini kwa ujumla mimi Vivi kama muuzaji
na mpambaji nimeona wateja wangu wengi zaidi wakipendelea wallpaper zenye
michoro kuliko zile za flati.
Zingatia kiasi cha mwanga kwenye
chumba husika kwa wallpaper ya rangi nzito au nyepesi ili kiwango kisiathirike iwe ni asubuhi, mchana au usiku.
Je ni
ukuta wa chumba gani unaotaka kuubandika wallpaper?
-Kama ni chumba
cha kulala cha wanandoa, wallpapaer zenye maua ndiyo zinafaa zaidi kwani zinaleta
hisia ya mahaba.
-Kama ni
sebule yenye mapambo ya mtindo wa kisasa, wallpaper zenye michoro ya rangi
nzito, metaliki, ya kung’aa na ya mguso wa mtelezo ndio zinafaa zaidi
kwani ndizo zinazoonekana ni za kifahari.
Swali lingine la kujiuliza ni kwa
staili unayotaka kubandika hiyo wallpaper. Staili zote hazileti muonekano
unaofanana, sawa eeh? Kwa mfano kubandika wallpaper kwenye ukuta mmoja tu kati
ya nne za chumba sio sawa na kubandika kwenye kuta zote pengine na dari. Chagua
wallpaper yenye rangi nzito kama unabandika kwenye ukuta mmoja tu mfano ule wa
luninga au wa tendego. Staili ya wallpaper yenye rangi za namna hiyo, metaliki
na mtelezo itatoa muonekano wa kiwango na kuvutia. Vilevile wallpaper za mtindo
huu zinapendeza pia kwenye dari.
Chumba kidogo kinapendeza wallpaper
isiyo na michoro au maua laa kama inayo basi yawe ni yale madogodogo. Wakati
kikubwa kikipendeza kwa wallpaper yenye michoro na maua makubwa. Na vilevile
kwenye kabati la maonyesho au vyombo likipendeza kwa wallpaper za rangi za
mwanga na moja.
Kwahivyo ukishakuwa na vigezo hivi kichwani, ni
rahisi kuchagua wallpaper sahihi.Tuna mitindo zaidi ya 100 ya wallpaper. Mawasiliano 0755 200023 tupo Sinza Kijiweni
No comments:
Post a Comment