Wanasema
kila safari moja kubwa inaanza na hatua moja ndogo. Na hata katika swala la
kubandika karatasi za kupendezesha kuta zijulikanazo kama wallpaper, hatua ya
mwanzo ndio yenye umuhimu mkubwa. Wallpaper hazishiki au kudumu kwenye kuta
zenye mafuta, chafu au rangi inayobanduka. Na ndio maana siwezi kuchoka
kusisitiza ni kwa kiasi gani ni muhimu kuandaa kuta vyema kwa ajili ya ubandikaji
wa wallpaper.
Kwa kuta
zilizopakwa rangi zamani
Hizi
ni zile kuta za zamani, yaani nyumba ambazo zilishapakwa rangi kitambo na
tayari watu wanaishi.
Endapo
lengo ni kubandika wallpaper kwenye kuta za aina hii hazitakiwi kuwa na rangi
zilizobanduka na wala maeneo yenye vinundunundu, nyufa au vishimo. Endapo maeneno
hayo yapo inabidi kuyaondoa kwa kukwangua na kurekebisha kwa kufuata hatua kama
zile za uandaaji kuta wakati unapotaka kupaka rangi ila unaishia kwenye hatua ya
primer ambayo huwa ni ya mwisho kabla ya kuanza kupaka rangi yenyewe. Kwa maana
hiyo panatakiwa pawe nyororo kabisa. Baada ya hapo ukuta wote usafishwe kwa
sponji au kitambaa kilicholoa ili kuondoa vumbi. Mara ukuta huu unapokuwa
umekauka ndipo ubandikaji wa wallpaper unapoweza kuchukua hatua.
Kwa kuta zenye
wallpaper ya zamani
Kuta
nyingi ni rahisi kufanyiwa maandalizi kuliko ambazo zilikuwa na wallpaper
tayari na unataka kuibandua ili kubandika mpya. Kwanza kabisa ni vyema ufahamu
kuwa ni lazima uondoe kwanza ile ya zamani. Mafundi wengi wanaobandika
wallpaper wanajua pia jinsi ya kubandua.
Kuta zenye ukungu
Ukungu unaweza kuonekana kwenye kuta
kwa rangi ya njano, kijani, kijivu au nyeusi. Kama hali hii ipo kwenye ukuta
unaotaka kubandikwa wallpaper paoshe kwanza kwa maji ya moto yenye blichi.
Paache pakauke kabisa halafu papake primer kabla ya kubandika wallpaper.
Pakishabandikwa wallpaper ukungu hauwezi kuota tena kwani wallpaper zilivyotengenezwa
haziruhusu ukungu kuota juu yake.
Kuta mpya
Endapo kuta/nyumba ni mpya na
umefikia kwenye hatua ya kupaka primer (kama tulivyosema huko juu katika
maandaliza ya kupaka kuta rangi) unachotakiwa ni kuepuka gharama mara mbili za
kupaka ukuta rangi ya mwisho halafu wakati huohuo unataka tena kubandika
wallpaper juu yake. Badala yake
unachotakiwa ni kuishia kwenye ngazi ya primer tu kwenye ukuta wowote unaotaka
kubandika wallpaper halafu badala ya ngazi inafuata ambayo ni ya mwisho yaani kupaka
rangi ndipo unabandika wallpaper.
Natumai msomaji
wangu umeelewa vizuri kabisa namna ya kuandaa kuta za aina mbalimbali endapo
unataka kuzibandika wallpaper.
Tunazo wallpaper za michoro zaidi ya 100. Wasiliana
nasi kwa namba 0755 200023
No comments:
Post a Comment