Zaidi wa wananchi 6000 wa kata ya wazo jimbo la kawe na
kata ya goba jimbo la ubungo jijini dar es salaam hawana mawasilaiano ya
barabara na huduma ya UMEME baada ya mto Tegeta kufurika maji na kusomba daraja
lao la muda walilokuwa wanategemea kuvukia na kusababisha shughuli za kata hizo
kusimama.
Wakazi hao wamethirika zaidi
kutokana na mto huo kufurika
maji huku ukiendelea kulika ukizifuata
nyumba za wananchi na wakazi wa mtaa wa muungano waliopo kata ya goba na mtaa wa kilimahewa waliopo kata wazo ambapo
ITV imeshuhudia wakazi hao wakilazimika kuhatarisha maisha yao kwa kutumia
kamba kwa ajili ya kuvuka huku nguzo ya umeme mkubwa ikiwa inaninyinia katikati
ya mto huo Jambo lilolazimu shirika la ugavi wa umeme nchini kakata huduma ya
umeme katika kata hizo.
Wakizungumza na ITV wakiwa wamefatana na mwenyekiti wao
wa mtaa wa muungano wananchi hao wamewalaumu vingozi wao wakiwemo wabunge na
viongozi wa wilaya ya kinondoni kwa kutowawekea daraja la kudumu katika mto huo
na kuwasababishia adha kila mara mvua kubwa inaponyesha ikwemo ya mwaka jana.
Wakazi wengine waliokubwa na mafuriko ni wanaoishi
kandokando ya mto mbezi ambapo nyumba zao zimesombwa na maji huku kingo za mto
huo zikiendelea kulika na kufuata nyumba zao ambapo wameiomba serikali
kuwapatia viwanja vya bei raisi sehemu nyingine.
Katika tukio lingine mvua zinazoendelea kunyesha
zimesababisha visima vya mafuta kujaa maji na kusababisha baadhi ya madereva wa
vyombo vya moto kukumbwa na adha kubwa
ya magari yao kuzima baada ya kuwekewa mafuta yalichanganyika na maji ya mvua
katika kituo cha mafuta cha kobil
kilichopo afikana huku meneja wa kituo hicho akisuasua kuwalipa madereva hao.
No comments:
Post a Comment