Monday, May 25, 2015

Madiwani washtukia ndoa feki za walimu...Baadhi ya walimu wa kike wanagushi vyeti vya ndoa kuwa wameolewa na wanawafuata waume zao mjini

BAADHI ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, wamesema tatizo la upungufu wa walimu kwenye shule za msingi zilizopo vijijini kunachangiwa na walimu hasa wa kike kutaka kufundisha mjini.

Walisema baadhi ya walimu wa kike wamekuwa wakighushi vyeti vya ndoa ili
kuonesha wameolewa na kuwafuata waume zao mijini jambo linalozorotesha jitihada za Serikali kumaliza tatizo la walimu kwani baadhi ya shule za vijijini zina walimu hadi wawili.

"Tatizo la walimu kwenye shule za msingi linatokana na walimu kujazana mijini hasa wa kike wakiwa na ndoa   bandia, madiwani tulitenga sh. milioni 30 ili zitumike kupeleka walimu vijijini lakini sijui mchakato huo umeishia wapi," 

Kwa upande  wake, Kaimu Ofisa Elimu wa Shule za Msingi wilayani humo, Stuart Kuziwa, alisema tatizo la walimu ni la kitaifa likiwemo la kujazana mijini lakini hata shule zilizopo mjini nazo zina upungufu wa walimu.

"Hata shule za mjini nazo zina upungufu wa walimu, tumeomba kupatiwa walimu 230 kwa miaka mitatu mfululizo, hilo linaweza kumaliza shida ya walimu katika shule za msingi," alisema.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Amir Kiroboto, alisema madiwani wasilalamikie tatizo la walimu kujaa mijini bali waangalie idadi ya wanafunzi kwani shule nyingi za mjini zina wanafunzi wengi.

MAJIRA

No comments:

Post a Comment