Monday, May 25, 2015

Mwigulu Nchemba Ajiuzulu

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Bw. Mwigulu Lameck Nchemba amejiuzulu kuanzia jana na nafasi yake kuchukuliwa na Mshauri wa Rais Jakaya Kikwete katika masuala ya Kisiasa, Bw. Rajabu Luhwavi.

Bw. Nchemba ambaye pia ni Naibu Waziri
wa Fedha na Mbunge wa Iramba Magharibi, alitangaza uamuzi huo Mjini Dodoma jana katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

Akizungumzia uamuzi huo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye, alisema Bw. Nchemba amechukua uamuzi huo ili aweze kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Alisema awali Bw. Nchemba alimweleza Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete juu ya uamuzi huo lakini rais alimshauri azungumzia jambo hilo kwenye kikao cha NEC.

Aliongeza kuwa, jana Bw. Nchemba alilifikisha suala hilo katika kikao hicho ambapo wajumbe wa NEC walilidhia aachie ngazi na kumtakia mafanikio mema katika mbio za kuwania urais na kumteua Bw. Luhwavi kushika nafasi hiyo.

MAJIRA

No comments:

Post a Comment