Thursday, May 21, 2015

Balozi Amina Salum Ali Ametangaza nia ya Kuwania Uraisi.......Amekuwa Mwanamama wa Kwanza katika Historia ya CCM Kutangaza Kuwania Uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

BALOZI wa kudumu wa Umoja wa Afrika (AU), huko Marekani, Mtanzania Amina Salum Ali, (Pichani) akitangaza jana Jumatano Mei 20, 2015, pale kwenye mgahawa wa Hadees jirani na askari monument, kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.

Balozi Amina ametangaza uamuzi wake huo mapema leo hapa hapa jijini Dar es Salaam.Itakumbukwa ya kuwa Balozi Amina ambaye alidumu kwa muda mrefu kama waziri kwenye serikali ya Rais mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour Juma, almaarufu kama (Komandoo), aliwahi kutupa karata yake kuwania urais wa Zanzibar, kabla ya kujitoa.

Huyu anakuwa mwana mama wa kwanza kwenye historia ya chama cha Mapinduzi CCM, kutangaza kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

VIJIMAMBO

No comments:

Post a Comment