Saturday, September 28, 2013

""vitu vizuri"" kutoka birthday party niliyohudhuria

kama kawaida napenda vitu vizuri. kwa hivyo nikienda mahali naangalia na kujifunza kwa undani vile vilivyonivutia. twende wote hatua kwa hatua tuburudike na kujifunza kutoka kwenye birthday party watu wangu wadogo waliyoalikwa.. karibu mdau..
safari inaanza


tukafika kwa mwenyeji wetu


buganvilia nyeupe zimechanua mno mno, ukiona utafurahi

nimependa huu ubunifu wa kuotesha maua ya kuzunguka ukuta wa fence. wengi huwa wanaotesha mstari wa kunyooka moja kwa moja ila huyu yeye karemba remba

rock garden
nikamuuliza mwenyeji wangu hiki chungu hapa juu ya rock garden ni cha nini? akaniambia kilikuwa kimeoteshwa ua lakini maskini limekufa!


michezo mbalimbali ya watoto ilikuwepo

keki

party people

marafiki zangu wa ukweli wakibembea
huyooo...nimejificha kwenye majani mapana


hapa na pale

ni mwaka mmoja na ushee tokea niamue kuwa mjasiriamali. kuna rafiki niliyekuwa nafanya naye kazi na imefikia muda anarudi makwao hivyo akanialika jana kwenye kimnuso cha kumuaga. nilichoshangaa hadi kwenye mabaa wanacheki mabomu siku hizi kutokana a janga la westgate. pia katikati ya kimnuso wacha nyoka aanguke toka kwenye mti...



hiki kiblauzi cha huyu mrembo ni mchanganyiko wa kanga na linen. kilinivutia hadi nikawa najiuliza hiyo nyeupe imeunganishwa ama ni kanga ikoje? ikabidi nimuulize. akaniambia mwanzo kabisa kilikuwa ni linen nyeupe tupu, hakukifurahia kuwa rangi nyeupe blauzi nzima. ndipo akaamua kukikata na kuweka kanga juu. nilifarahia mno ubunifu wake!



tuwe makni tunapokuwa mahali kwenye miti, nyoka huyu alianguka toka mtini!

nikiwa na mwenyeji wangu Sabina.

Friday, September 27, 2013

vitu vizuri...

tazama kazi mbalimbali za sanaa ambazo unaweza kutumia kama mapambo ya ndani kadri uwezavyo kubuni. nyingi unaweza kuziweka kwenye display cabinet la sebuleni




ceramic zenye mfano wa maumbo mbalimbali ya ndege




jewelry

hii ceramic yafaa haswaa kwenye kabati la urembo

vikapu kwa maumbo mbalimbali

friday finest

hili jani la canadian asikuambie mtu linapendezesha mno bustani. unaweza dhani ni zulia la kijani limetandikwa nje. huwa linafunga kiasi kwamba hata magugu ni machache sana. kazi ni kumwagilia na kuweka mbolea ya kuku hasa wakati wa mvua ili kusaidia kung'arisha ukijani. kama una bustani hata kama ya hatua kumi na umeotesha pemba grass ondoa uoteshe haya ya canadian. ukitembea bustanini hata kama umevaa soksi huchafuki. Onyo: usijedanganyika na yale ya Mwanza ambayo yanafanana sana na haya ya canadian ila kwa ubora hayafikii canadian.

Thursday, September 26, 2013

My article for newspaper: Namna ya kuandaa kuta kwa ajili ya kupaka rangi

Kuandaa kuta kwa ajili ya kupaka rangi ni hatua muhimu kwa kazi hiyo kubwa. Kile kitendo cha kupaka rangi kinachukua muda mfupi sana na sio muhimu kama hii kazi ya maandalizi ya kuta. Ingawa unaweza kuwa na shauku ya kuona matokeo ya mwisho yaani rangi mpya imepakwa lakini kama hutafuata hatua muhimu za kuandaa kuta kabla ya kitendo cha kupaka rangi, kazi yako ya kupaka rangi inaweza kugeuka majanga.


Hatua ya kwanza ya kuandaa kuta zako kabla ya kupaka rangi ni kuondoa fenicha zote ambazo zinahamishika kirahisi kutoka kwenye chumba. Funika kwa vitambaa zile kubwa ambazo huwezi kuondoa au kusogeza. Ondoa kila kinachowezekana kwenye ukuta kwa maana ya labda umetundika mapambo ya picha na fremu pamoja na taa na vishikizo vyake. Ili upunguze maeneo ya kuweka tepe kama itawezekana pia ondoa swichi za taa na vitasa vya milango ambayo hutaipaka rangi. Hii itafanya upakaji rangi uwe rahisi na kupunguza kazi ya kufunika vifaa hivi. Kumbuka kuzima umeme wakati ukiondoa swichi na taa. Tunza vimisumari na sukuruu vizuri kwenye mfuko mdogo na hata ikiwezekana ziweke alama. Rangi zinadondoka kwenda chini kwahivyo hakikisha kila kilichopo chini ya eneo unalopaka rangi kimeondolewa au kimefunikwa. Pia matone mengine ya rangi yanaweza kwenda upande upande kutegemea na jinsi mpakaji anavyochakarika na kazi yake hivyo hakikisha walau eneo la mita mbili linalopakwa rangi vitu vyote vimefunikwa au vimeondolewa.

Ukishakuwa sasa umeondoa vitu utaziona kuta vizuri kwa uwazi kwa hivyo hatua inayofuata ni kuziba nyufa, matundu na kukwaruza maeneo rangi ya zamani ilikovimba au inakobanduka. Kufanya marakebisho haya ni muhimu sana kabla ya hatua ya kupaka rangi. Utatakiwa kutandaza makaratasi ya plastiki chini kabla hujaanza marekebisho haya ili kuzuia vumbi na uchafu wa mchanga usichafue hasa kama sakafu ni ya zulia  la ukuta kwa ukuta. Kazi hii ya marekebisho sio ya kupuuza inabidi kuwa na fundi anayeelewa kazi yake kwani inatofautiana sana kitaalam kwenye kurekebisha tuseme nyufa, matundu na kona zilizovunjika.
Baada ya hapo hatua inayofuata ni kuhakikisha sehemu zilizofanyiwa marekebisho zimekauka na fundi atumie kitambaa kufuta vumbi kwenye yale maeneo yote aliyorekebisha. Hii ni muhimu kwani rangi haishiki eneo lenye vumbi. Kama kuna eneo limeota ukungu, lisafishwe kwa maji na hakikisha ukuta unaachwa ukauke ili kuzuia ukungu kujitokeza tena hapo baadaye. Kuna dawa za utangulizi (Primers) ambazo zinasaidia kuzuia ukungu na fangasi.
Hatua inayofuata ni kujiridhisha kuwa kuta ni safi hazina chembe ya vumbi wala utando wa buibui na ni kavu. Unatakiwa uwe unaweza kufuta ukuta na sponji bila chochote kudondoka toka ukutani. Kama kuna rangi ya zamani ambayo inatoka itatakiwa kukwaruzw tenaa ili itoke, laa sivyo rangi mpya utakayopaka juu yake nayo itaanza kubanduka mapema.
Sasa kuta zako ni safi, kinachofuata ni kufunika kwa kuweka utepe maeneo yote ambayo hutaki yashike rangi. Kama umeondoa zile swichi za taa kama nilivyoelekeza mwanzoni basi utakuwa na sehemu chache sana za kufunika. Hata hivyo bado itakubidi kufunika fremu za madirisha na pembeni mwa vitu vya mbao ambavyo hutaki vishike rangi ya kuta. Tepe za mpaka rangi zimetengenezwa maalum kwa kazi hiyo na gundi yake haifanyi uharibifu wakati wa kuondoa.

Hatu inayofuata  ni kupaka dawa ya utangulizi kwenye yale maeneo ambayo yamefanyiwa marekebisho. Kumbuka hapa tunaangali kuta ambazo tayari zilishapakwa rangi zamani na sio kuta mpya. Kama zingekuwa kuta mpya basi hii dawa ya utangulizi ingepakwa kuta zote kabla ya kupaka rangi. Hi inasaidia kuleta matokeo mazuri kwani dawa ya utangulizi inasaidia kuweka mshikamano na rangi kwa hivyo pia kusaidia kupunguza gharama kwani inahitajika mizunguko michache ya rangi kukiwa na dawa ya utangulizi.
Mara unapomaliza hatua hizi chache muhimu za utangulizi, sasa uko tayari kupaka rangi! Ingawa kazi ya maandalizi ya kuta kabla ya kupaka rangi inaweza kuonekana kubwa, matokeo ya mwisho ni mazuri na nguvu iliyotumika inalipa!

Paka rangi! Weka mizunguko mingi iwezekanavyo hadi ukuta uonekane maridadi na kuwe na ulinganifu wa eneo lote kwa maana ya kwamba kusiwe na mawimbi mawimbi. Kwa rangi ya ubora wa juu unapaka mizunguko michache (miwili au mitatu tu) na kupata matokeo mazuri.
Umeshamaliza kupaka kuta zako rangi na zimeshakauka, sasa ondoa zile tepe. Kama kuna rangi kidogo imevujia chini ya hizi tepe chukua kibrashi kidogo na uguse maeneo hayo kwa uangalifu usije ukachafua kwingine.
Baada ya mzunguko wa mwisho wa rangi kukauka kabisa, anza kurudishia vile vitu vya ukutani kama swichi na sanaa zako za fremu ulizokuwa umeondoa ikifuatiwa na kurejesha fenicha na kila kitu mahali pake. Sasa umemaliza kupamba kwa kupaka rangi, kilichobaki ni kusherehekea!

Kuamua kuwa unataka kupaka upya rangi makazi yako inatakiwa uwe na muda wa kutosha. Fikiria kama una watoto wadogo na wanyama wa ndani kama vile paka watakuwa wapi kipindi cha maandalizi na kupaka rangi. Kumbuka utakuwa unaangalia kuta hizi kwa muda mrefu na hakikisha utafurahia mradi huu uliosimamia.

Makala hii imeandaliwa na Vivi O. Machange. Vivi ni mjasiriamali upande wa usafi wa mazulia, nguo na magari; pia ana mapenzi makubwa ya mitindo na mapambo ya nyumbani. Kwa maoni au maswali tuma kwenda 0755 200023 au viviobed@yahoo.co.uk

Wednesday, September 25, 2013

mid week miscellaneous





jani limekubali, nam quote Maya Angelou “If the grass looks greener on the other side, you can bet the water bill is higher.”

Tuesday, September 24, 2013

pumzika kidogo

kwa wale wa masaa ya kazi ya day, siku karibia inayoyoma kwa hivyo relax kidogo kwa kuangalia picha hizi nzuri...vitu vizuri....
mrs. O na mumewe

una enjoy bustani kama hivi

dakika ya ukimya jumba jeupe wakati wa kukumbuka 9/11. Mungu warehemu marehemu

jengo ni mawe!

kunong'onezana kama hivi


nyumba hii ina mazingira rafiki kwa watoto

vitu vizuri havina kikomo, mazingira ya nyumba hii yanaweza ku prove usemi huu. kama wewe ni mmoja wa wanaoanza familia au una familia changa unaweza kubuni mapambo ya ndani ya nyumba yako kadri upendavyo kwani ukiwa na watoto wadogo wanafurahia zaidi mazingira rafiki kwa umri wao na wakati huo huo ukibakia kuwa stylish. usiogope rangi, unaweza kuweka pinki, nyekundu, kijani ya limao na kadhalika uamuzi ni wako, ladha ni yako na makazi ni yako.
makabati ya jikoni ya pinki na trash can za kijani na njano

ona sanaa ya ukutani imewekewa na kibuyu cha shanga, watoto wanafurahia kuona vitu kama hivi

rangi kila mahali

Monday, September 23, 2013

fenicha za nje ya nyumba

fenicha za kwenye bustani kwa hapa kwetu zaweza kuwa za mbao ngumu kwa maana ya mkongo na mninga kwa vile zitaweza kupambana na shurba nyingi kama jua kali, mvua na upepo. pia zaweza kuwa za chuma ili mradi ukipake dawa ya kuzuia kutu ama zaweza kuwa za aluminium. fenicha kama hizi hapa chini japo picha ni ya mazingira ya nje ya TZ lakini nawe waweza kuwa nazo kwenye makazi yako kwani malighafi zote za kutengenezea zinapatikana hapa nyumbani. mradi kitu roho ipende..
hivi viti waweza kutengeneza kwa mbao ya mninga ama mkongo. mito inapatikana kirahisi kama kufumba macho na kufumbua. wakati mito haihitajiki toa hifadhi stoo, rangi zake za kuwaka zinasaidia kuongeza rangi na kufanya sehemu ivutie. hiki kimeza tengeneza kwa chuma na juu yake weka kioo kwa urahisi wa kusafisha na ili kidumu kama hapa alivyoweka..

poleni sana Wakenya: kwa jirani ni kusafi

inasikitisha ambapo mtu unaamka mzima na kujiendea zako kufanya shopping mall lakini kwa kisirani unakutana na kifo au ukilema kama ilivyotokea kwa jirani zetu Kenya kwenye westgate mall ambako kwa uchache watu 68 wameuawa na 75 kujeruhiwa. hata hivyo kwa ajili tunajifunza kila siku nimekuwa nikiangali tukio hili na kuona jinsi jirani yetu alivyo msafi kwenye jiji lake. haijalishi kuna kiongozi gani mashuhuri duniani anayemtembelea..tehe tehe teh bali ni makazi yake kila siku ndivyo anavyoishi. poleni sana Wakenya ila waTz tuna cha kuiga kutokana na unadhifu wa mazingira ya jirani. 
ona bustani zilivyo kuwa pruned vizuri, chini hamna hata sisimizi. hapa wabongo hawakawii kujitetea oh hali ya hewa ya Nairobi inaruhusu...hamna lolote siasa nyingi kuliko kazi

ona palm zilivyonawiri, ukijani unafurahisha

unaweza desa hizi grill, ukapeleka kwa mchomeleaji akakutengenezea kama hivi

kila mahali ni nadhifu! big up jirani

Saturday, September 21, 2013

muonekano wa jiko dogo

nimefanya utafiti kutaka kujua wasomaji wanavutiwa na nini hasa kwenye blog hii. katika findings  zangu kwa kuangalia nyenzo za trafiki nimegundua kuwa wasomaji wengi wananifikia kwenye blog kutoka search engine za google na yahoo wakitaka kujua zaidi kuhusu jikoni kwa ujumla kwa maana ya makabati, mpangilio wa jiko na kadhalika. kwa hivyo ninakata kiu yao kwa ku share picha hizi chache za at least jiko dogo la kisasa linavyotakiwa kuwa na vitu vyake muhimu. enjoy!
jiko dogo lililokamilika. kila eneo limekuwa utilized. juu ya hii kaunta yenye vyombo kwa chini watu wanaweza kukaa na kula

stovu ambayo yaweza kuwa na pande 2. upande wa kutumia gesi na wa umeme. halafu mwenye jiko lake kaamua kupanga kwa kuweka microwave juu ya stovu. nadhani ni ili kutumia vyema eneo dogo alilo nalo

sehemu ya kuhifadhia viungo vya chakula. kumbuka hivi havina haja ya kuweka ndani ya friji

droo la vitambaa na vitaulo

friji la kisasa

tosta, jagi la miko, vipawa na vijiko vikubwa na vibao vikiwa juu ya kaunta


shelfu za vyombo za wazi zilizo karibu na dirisha, kwenye hizi kabati za chini yake hifadhi masufuria na vikaangio

sinki na kichujio chake cha kati. juu yake kutakuwa na bomba za maji moto na baridi. chini ya kabati zilizobeba sinki weka vifaa vyako vya usafi kama sabuni na sponji