Kosa dogo tu katika
uwekaji wa marumaru sakafuni au ukutani kwa jikoni na bafuni linaleta ukakasi
machoni. Marumaru moja tu inapokuwa imewekwa vibaya , inaweza kuharibu mtiririko mzima na kufanya
muonekano wa kupinda. Mbaya zaidi kufanya marekebisho baadaye, inaweza kuwa
gharama,
usumbufu na kuchafua maeneo mengine. Gharama inahusika hasa pale inapotokea
toleo lile limeisha madukani na kuweka “kiraka” hutaki.
Ndio maana ni muhimu ukiwa
na kazi ya kusimika marumaru uwe na fundi sahihi anayeweza kufanya kazi iliyotukuka
toka mwanzo, kwa maana ya kusionekane makosa baadaye.
Nimeongea na mkandarasi
Sood Domwa na akatoa dondoo zifuatazo za jinsi ya kuweza kumpata fundi marumaru
mzuri. Bwana Sood anasema marumaru ni bidhaa ngumu sana
kwamba huwezi kuifanya kwa namna yoyote ile ibonyee. Hata hivyo pamoja na ugumu
wake ni rahisi mno marumaru kuvunjika. Hivyo basi ili kuzuia marumaru
zilizokwisha simikwa sakafuni zisifanye mipasuko ni muhimu kuhakikisha hakuna
nafasi kati ya marumaru na sakafu iliyo chini yake. Yaani marumaru inatakiwa
ishikane kabisa na eneo lililoibeba. Nafasi wazi chini ya marumaru itasababisha
marumaru kukunjika pale ambapo uzito wa mwili unakaa juu yake mtu anapoikanyaga
akitembea na hivyo kuifanya ivunjike.
Kutokana na haya yote ndipo tunasema ni muhimu kupata
fundi wa viwango kwa kutumia dondoo hizi:
Uliza wakandarasi
Kuna uwezekano mkubwa wa kumpata fundi mzuri wa kuweka marumaru kutoka kwa wakandarasi. Hii ni kwasababu kazi kubwa za kuweka marumaru ziko kwenye majengo makubwa ya biashara, na wakandarasi wanavutiwa zaidi na kazi za namna hiyo kuliko hizi ndogondogo za nyumba za kuishi. Kwahivyo kuongea na mkandarasi kwako wewe unayejenga nyumba ya kuishi kutakupa uwezekano mkubwa wa kukupatia fundi mzuri wa marumaru. Pia kama utafanikiwa kupata mkandarasi aliyeko tayari kufanya kazi yako ndogo itafaa zaidi, sababu ikiwa ni ile ile kuwa wana uzoefu mkubwa wa kuweka marumaru kwenye majengo ya biashara. Na sikuzote mwenye nyumba kataa kuchukua fundi wa kuweka marumaru kutoka vibarua.
Fundi marumaru wa kufanya
kazi yako anatakiwa kuwa na uzoefu wa kazi hiyo usiopungua miaka mitatu, muulize
akuonyeshe kazi zake. Na kuangalia picha tu ya kazi za nyuma hakutoshi- picha
zinaweza kudanganya. Sisitiza kuona angalau eneo moja alilosimika marumaru.
Uliza kwa Wauzaji
Wauzaji wengi wa marumaru wanawajua mafundi wazuri na kuna wengine wanao mafundi wao kabisa. Pia mafundi wengi wanapenda kutengeneza urafiki na wauzaji ili wawe wanawaitia wateja kwa maana ya wao mafundi wapate kazi.
Wauzaji wengi wa marumaru wanawajua mafundi wazuri na kuna wengine wanao mafundi wao kabisa. Pia mafundi wengi wanapenda kutengeneza urafiki na wauzaji ili wawe wanawaitia wateja kwa maana ya wao mafundi wapate kazi.
Hakiki Ubora
Wakati unapoangalia kazi za fundi alizofanya kabla, fahamu kwamba uwekaji marumaru hautofautiani kuendana na ukubwa. Angalia ulingano wa ile nafasi kati ya marumaru moja na nyingine na pia hakikisha ile mistari ya grauti imelingana na kunyooka vizuri kabisa.
Angalia jinsi marumaru
zilivyotandazwa. Je, kuna uwiano? Fundi mzuri anaanzia kati kati ya chumba ili
vile vipande vya kuweka maeneo ya mwisho ya ukutani vikae vizuri na kwa ukubwa
sawa. Pia tazama nyuma ya milango kwenye kona na kona zozote za kipekee
zinazoweza kuwa kwenye chumba. Kwa ajili marumaru za kukata ni changamoto kwenye
maeneo hayo, ni kielelezo kizuri cha ujuzi wa fundi. Hakikisha kuwa marumaru
zinazozunguka fremu ya milango zimekaa vizuri laa zitafanya bonde au kuacha
nafasi maji yasimame. Kama ni za ukutani angalia yale maeneo yenye bomba.
Hakikisha kila mahali pamezibwa vizuri.
Usafi wakati wa uwekaji
Njia nyingine ya kupata fundi sahihi ni kwa kumuuliza mwenye nyumba aliyefanyiwa kazi na fundi
husika juu ya swala la usafi. Fundi anayefanya kazi ya marumaru kwa uchafu
anachangia kuacha alama za kudumu sakafuni. Kwa mfano saruji ikishakaukia juu
ya kioo cha marumaru zenye vishimoshimo huwa haitoki tena.
Gharama
Mafundi wengi wa kuweka marumaru wanapendelea kuchaji kwa
mita za mraba. Na endapo wakianza kufanya kazi na ukajikuta kuwa muonekano
uliotokea sio uliokuwa nao kichwani, utakuwa hujachelewa kama utabadili wazo
mapema. Ila huenda ukaishia
kulipa gharama mara mbili za kuondoa hizo ambazo zilishaanza kuwekwa tayari. Na
ndio sababu ni muhimu kufikiria mapema kuhusu michoro na maeneo
zinapochanganywa za rangi tofauti ili
kuondoa kadhia ya kurudia.
No comments:
Post a Comment