Naomba ingia instagram @mtotomagazine u like picha hii hapa chini ili ishinde. Asante sana
Moja
kati ya maswali ambayo wengi wanaotaka kununua kitanda wanajiuliza ni kama
wanunue cha mbao au cha chuma. Aina zote mbili zina faida na changamoto zake
kama ifuatavyo.
Andrew
Komba wa kampuni ya Furniture Mart iliyoko Tabata
simu 0655 974 223 anasema kuwa fremu za mbao
kwa ajili ya kitanda ni
imara na salama zaidi kuliko za chuma. Ni salama kwakuwa finishing yake haiachi ncha kali zinazoweza kuleta madhara ukilinganisha na cha chuma.
imara na salama zaidi kuliko za chuma. Ni salama kwakuwa finishing yake haiachi ncha kali zinazoweza kuleta madhara ukilinganisha na cha chuma.
Kwa
kawaida ya binadamu toka enzi, kitanda cha mbao kinampa mlalaji hisia za
burudiko kuliko cha chuma, na pia kimapambo, kitengeneza mandhari ya
kupendezesha chumba zaidi hasa kama kimetengenezwa kwa mbao ngumu na zenye
rangi za asili. Mbao za mninga na mkongo zinakifanya kitanda kionekane cha
kifahari na kinakipa chumba muonekano wa uhalisia, utulivu na ukamilifu.
Komba
anasema, kitanda cha mbao ni bei nafuu ukilinganisha na ubora na uzuri
unaotokana nacho. Usidanganyike kwa kutazama wakati wa kukinunua kuwa bei ni
kubwa kwani ukweli ni kwamba kitanda cha mbao kinakupa garantii ya pesa zako
hadi zaidi ya miaka 30 mbele. Ni kama umewekeza na ikitokea wakati wowote
unataka kukiuza kutokana na sababu yoyote ile labda unahama mkoa, au unataka
kikubwa zaidi ni kwamba thamani yake inaongezeka.
Kitanda
cha mbao kinaweza kuwekwa urembo wa aina mbalimbali na pia kutiwa rangi kwa
jinsi ambayo uzuri na michoro ya mbao bado inaonekana katika uhalisia wake. Au kwa mitindo
ya siku hizi ambapo hupakwa rangi na kuleta muonekano na mguso tofauti kabisa
kama vile tunavyoviona kwenye rangi nyeupe au nyeusi za mati.
Kitanda
cha mbao ni imara na hakina kelele kwakuwa mfumo wake wa kukifunga hautumii
sukuruu za chuma ambazo hulegea baada ya muda mfupi.
Komba
anasema kwa uzoefu wake na wateja wake ni kwamba kitanda cha mbao kina utulivu
zaidi kwa usingizi ukilinganisha na kile cha chuma ambacho kinaweza kuwa na
kelele na kisikupe usingizi mwororo, na pia fremu ya mbao inalifanya godoro
litulie kitandani.
Ni
rafiki wa mazingira, kwani unaweza kuitumia mbao hiyo tena na tena kwa manufaa
mengine na pia miti inayotumika ni nishati mrudio ambayo inaoteshwa na kuota
tena.
Kimuonekano
vitanda vya mbao vinavutia na vina muonekano wa asili kwa sababu vinatengenezwa
kutokana na miti ambacho ni kitu hai.
Ni
rahisi kukitunza na kukifanyia marekebisho endapo kuna uharibifu umetokea.
Kutokana
na uchambuzi huu ni matumaini kuwa itakurahisishia kufanya uamuzi pale
unapotaka kununua kitanda, na kama ni cha mbao nunua cha mbao ngumu tofauti na
cha bei rahisi kisichokuwa cha mbao halisi bali mabaki ya mbao. Vitanda
vilivyotengenezwa kwa mabaki ya mbao baada ya muda vina hatari ya kuumuka na
hasa pale vinapokutana na maji ndio mbaya zaidi, usidanganyike na muonekano
wake wa kuvutia.
No comments:
Post a Comment