Kuna cha ziada katika
kuchagua muonekano wa ukuta wa nje wa nyumba badala ya kuamua tu kupaka rangi
nyeupe kwa mfano. Kwa nyakati za sasa wenye kujenga wengi wanapendelea
kuweka kuta za nje za nyumba zao katika
hali ya ukisasa zaidi. Mbali na rangi laini za kawaida zilizozoeleka toka zamani ambazo ni maarufu
kwa kuta za ndani, kuna rangi mpya nyingi za nakshi kwa ajili ya
ukuta wa nje wa
nyumba.
Ahmed Salim ambaye ni
mtaalam wa nakshi hizi kutoka Aqua Deco Kijitonyama 0712 792 909 anatujuza kama ifuatavyo, twende tuelimike pamoja
msomaji wangu.
Tunaangalia aina 4 za
rangi za nakshi kwa ajili ya ukuta wa nje wa nyumba. Nyingi ya nakshi hizi ziko
rafu jamii ya mawemawe ambazo kwa majina ni drewa, silkoretasit, crystone na
wallmaster. Nakshi hizi nne zimetengenezwa maalum kwa ajili ya ukuta wa nje kwa sababu zina uwezo
wa kustahimili hali ya hewa yoyote na zinadumu kwa zaidi ya miaka 15. Kati ya
hizi aina 4 zinazopendwa zaidi Tanzania kwa sasa ni drewa, wallmaster na crystone.
Drewa ni nakshi za
mawe makubwa ya asili yaliyosagwa na kuzalisha mawe madogodogo mithili ya
ukubwa unaozidi kidogo punje za mchanga wa mtoni. Nimetofautisha kabisa kwa kusema mchanga wa
mtoni kwani michanga mingine kwa mfano wa baharini una punje ndogondogo sana.
Vimawe hivyo vinakuwa vimegandishwa pamoja na kutoa muonekano wa rangi kwenye
picha kubwa. Watanzania wengi wanaojenga nyumba za kisasa wanaonekana
kupendelea drewa kwenye kuta za nje.
Nakshi ya silkoterasit
ikipakwa/bandikwa ukutani inafanya muonekano mlaini na rafu. Yale maeneo laini
yana mng’ao.
Crystone ni malighafi za punje zilizotokana na
mawe yaliyosagwa, kwakweli inapendeza, itakuondoa katika hali ya kupaka rangi
jengo lako mwaka hadi mwaka.
Tofauti na drewa ni kwamba japo ukuta unakuwa na nundunundu lakini mguso wa juu
ni mlaini. Crystone Ina kemikali za kuzuia fangasi na inadumu hadi miaka 25.
Bila shaka msomaji wangu utakuwa umeona nyumba zilizopakwa nakishi hii ya crystone.
Wallmaster ni nakshi ambayo malighafi yake ya
awali inakuja kwa mfumo wa unga. Kimuonekano inakaribiana na silkoterasit.
Kwa hivyo kwa hizi
nakshi 4 ziko kwenye jamii ya rangi nyingi mno zaidi ya 100, yaani kwa mfano
nakshi ya drewa unaikuta kwenye rangi mbalimbali vivyohivyo na nakshi zingine 3
zilizobakia. Kwa maana hiyo kabla hujachagua rangi ya nakshi chukua muda
kutafakari muonekano unaotaka. Kuna mwenye nyumba ambaye anapendelea kupaka
ukuta wote nakshi ya rangi moja, na kuna ambaye anapendelea kupaka sehemu kubwa
ya ukuta rangi moja halafu kwenye kona, msingi na kuzunguka madirisha akapaka
nakshi ileile lakini kwa rangi nyingine. Hii
ni ili tu kufanya nyumba ivutie kwa ladha yake mwenye nyumba anavyotaka.
Mara nyingi inategemea pia na jinsi usanifu wa nje ya nyumba ulivyo. Kuna
nyumba kwenye ujenzi kona zinakuwa tayari zimeshanyanyuliwa kuliko maeneo
mengine. Kama ndivyo, basi kupaka nakshi ya rangi tofauti na ile ya ukuta mzima
huwa inaleta mvuto.
Vilevile kwenye
kuchagua rangi ya nakshi unatakiwa
kuangalia mazingira mengine ya nje. Huenda maua, miti na ukoka umezidisha sana
kijani. Unatakiwa kuchagua rangi ambayo itatawala hicho kijani.
Vivi anakuwezesha kupendezesha
nyumba yako. Simu 0755 200023
No comments:
Post a Comment