Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
TFF iliyoketi jumanne tarehe 5 Mei, 2015 imempiga faini ya sh. 5,000,00
(milioni tano), Afisa Habari wa klabu ya Yanga SC Jerry Muro kwa kutoa kauli za
chuki, kisirani na uchochezi dhidi ya uongozi wa Bodi ya Ligi (TPLB) nchini na
TFF.
Akitoa utetezi wake mbele ya Kamati ya Nidhamu, Jerry
Muro alikiri na
kujutia kufanya kosa hilo na kudai ilitokana na ugeni wake
katika uongozi wa michezo, kwa kuzingatia hilo kamati ilimuepusha na adhabu ya
kufungiwa..
Kwa mujibu wa Ibara ya 53 (2)ya Kanuni za Nidhamu za TFF
toleo la 2012, kwa kuidhalilisha TFF na Bodi yake ya Ligi mbele ya umma, kamati
imemtoza faini ya sh. 5,000,000 (millioni tano), Jerry Muro na kuwaonya
viongozi wengine wa familia ya mpira wa miguu kutojihusisha na vitendo vya
matamshi ya aina hiyo.
Shitaka linalomhusisha mchezaji wa Yanga, Amissi Tambwe
kumshika kwa kumdhalilisha mchezaji wa Simba SC Juuko Mursheed, na kiongozi wa
Friend Rangers Hery Chibakasa wa Friends Rangers kuhamasisha vurugu katika
mchezo wa timu yake na dhidi ya Majimaji ya Songea Januari 29, 2015, kamati
imeahirisha mashitaka hayo mpaka tarehe nyingine itakapopangwa.
Kamati iliahirisha malalamiko dhidi ya Mohamed Hussein,
Muhibu Kanu, Manfred Luambano, Venance Joseph, Mussa Senyange, Saleh Ali,
Shafii Maganga na Ismail Salim baada ya kupokea taarifa za udhuru
zilizosbabishwa na mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria ya mikoani.
No comments:
Post a Comment