Monday, October 14, 2013

Sunday, October 13, 2013

mvua hiyoo.. anza kusafisha mifereji

unaweza usiwe na gutter kama hizi kwenye picha, ila kinachojalisha ni mfereji wake. kama mfereji umejaa majani na tope ni rahisi kusafisha mwenyewe, chukua ngazi uanze kusafisha. ila kama nyumba ni ya ghorofa inaweza kubidi kuita mtaalam.

taa za njia ya miguu

habari  mbaya ni kuwa giza linaingia mapema kiasi kwamba huwezi ku enjoy bustani yako. habari njema ni kuwa unaweza ukaweka taa za kwenye bustani ili kwenda kitandani muda unaotakiwa. njia rahisi zaidi ni kuweka taa za solar. 

Friday, October 11, 2013

wapambaji igeni hii

amini usiamini maboga yanaweza kupindua ulimwengu wa upambaji wa kwenye shughuli. iwapo boga litakuwa kwenye msimu na una shughuli yako acha kutumia vesi na roses tumia maboga kama hivi!!
wageni watafurahije? utapata soko hapo hapo kama wewe ni mpambaji

boga linapogeuka flower vase

unaweza ukaliandika chochote

hapa unalitoboa toboa halafu unachomekea maua

vase nyingine hizo usikimbizane na machupa wakati ni msimu wa maboga

hata shada linawezekana


nimebamba bustani nyingine ya mawe

hii hapa toka sehemu ya wazi ndani ya jengo refu la biashara. ina muonekano mzuri ukiwa ndani ya ofisi kwani unaiona kwa dirishani karibu kabisa. wa tz wako juu!

fabulous friday

weekend inaanza mdau..usikubali mtu akuibie furaha yako...







Thursday, October 10, 2013

nyumba sio lazima iwe kubwa kinachotakiwa ni unadhifu

nimeshangaa nyumba hii (structure ya kawaida kiasi) ya billionaire wa microsoft niliyokutana nayo mtandaoni aliyonunua hivi karibuni eti!

jengo lenyewe

majirani ni mabilionea wenzie
jiko la kupikia mahanjumati yake, familia yake na wageni wake

sebule na feni zake! sare sare maua kizulia cha jikoni na cha coffee table


eneo la farasi  wake kujidai
picha kwa hisani ya zillow

My article for newspaper: Feni

Zaidi ya kuleta ubaridi na matumizi nafuu ya nishati na pesa, feni pia ni pambo la ndani

Wakati wa majira ya joto, ni ngumu kukaa ndani na kujisikia burudani, starehevu na amani  bila kupandisha bili ya umeme. Wakati huo ndipo kila mmoja anahangaika ni kwa vipi aweze kumudu ndani kuwa na ubaridi. Kwa bahati nzuri suluhisho ni rahisi zaidi ya kuwekeza kwenye kiyoyozi. Ingawa kwenye maeneo mengine ya nchi kiukweli ni kuwa wakati wa joto kiyoyozi kinahitajika kwani kwa kawaida maeneo hayo joto huwa ni kali sana. Lakini pale unapotaka kuweka chumba kimoja kipoe kidogo feni inaweza kuwa ni suluhisho.

Ni muhimu kujua kuwa feni haipunguzi joto ila inatengeneza mpepea ambao unamfanya mtu asikie ubaridi kwani mpepea huo unasaidia kuvukiza jasho toka kwenye ngozi ya mtu huyo. Ni hisia hiyo hiyo unayopata pale unapofungua kioo cha gari likiwa linatembea. Kuweka feni kila chumba ambacho watu wanakaa inasaidia wanafamilia kupooza miili wakati wa joto wakati huo huo ikiwa ni matumizi nafuu kipesa kulinganisha na kiyoyozi. Teknolojia imewezesha kuwa na aina za feni za matumizi madogo sana ya nishati kulinganisha na miaka ya nyuma. Tafiti zinasema kuwa feni inaweza kuwasaidia wenye nyumba kupunguza matumizi ya nishati kwa hadi asilimia hamsini ya ambayo ingekuwa bili ya kiyoyozi kwa kutengeneza mpepea ambao unafanya joto kuwa chini kwa nyuzi 7  hadi nane za sentigredi kuliko ambavyo ingekuwa bila feni wala kiyoyozi.

Feni zipo za kwenye dari, za mezani, za sakafuni na za ukutani. Feni hizi zinatengeneza mzunguko wa upepo ambao unakuweka burudani zaidi nyumbani kwako, hata kama una vipoozeo vingine kama uingiaji ndani wa hewa ya asili au kiyoyozi.
Feni ya kuning’iniza darini inachukuliwa kuwa ndio yenye ufanisi zaidi kwa kuzungusha hewa kwenye kila eneo la chumba.  Pia feni ikiwashwa pamoja na kiyoyozi inasaidia kupunguza matumizi ya umeme kwani unasetia kiyoyozi kwenye fukuto la juu kwa kuwa feni inakuwa imeshaleta mpepea tayari (ukisetia kiyoyozi kwenye fukuto la chini ndivyo kinavyokula umeme mwingi).

Feni za darini zinatakiwa kufungwa sehemu ambayo ukuta wake una urefu wa si chini ya futi nane ili mapanga yake yaweze kufanya kazi vizuri. Feni zenye mapanga makubwa zinazungusha mpepea zaidi ya zenye mapanga madogo. Pia mapanga makubwa yanafanya kazi nzuri kwa kasi ndogo kuliko madogo. Ukubwa wa feni uendane na ukubwa wa chumba, kama chumba ni kikubwa kwa mfano sebule, weka feni zaidi ya moja. Feni izimwe wakati ukiondoka chumbani kwani inapooza ngozi za watu na sio chumba.  Kwa nyumba kubwa, kufunga feni ndogo ya darini kwenye chumba cha kufulia na chumba cha kuvalia si jambo la ajabu. Kwenye bafu za wakuu wa familia pia ni mahali sahihi pa kufunga feni ndogo kwani mvuke wa maji ya moto na vikausha nywele vinaweza kufanya bafu liwe na joto na mnato. Kifeni kidogo cha darini kitaleta burudiko mahali hapo.

Feni ya bei kubwa inafanya kazi kiufanisi, kiulaini na kimya kimya zaidi ya ile ya bei ndogo. Hakikisha kiwango cha kelele kilichoandikwa kwenye feni kabla ya kuinunua na kama itawezekana isikilize ilifanya kazi kabla ya kuinunua. Na pia nunua feni yenye lebo inayoonyesha matumizi ya nishati kwani feni ya aina hii ina ubora kuliko ile isiyoandikwa chochote. Pia hakikisha kwamba feni unayotaka kununa ni ya mazingira ya nje au ndani ya nyumba, kwa mfano feni ambayo imeandikwa ni ya ndani haitakiwi kutumika nje – hata kama eneo limezibwa sana. Unyevu na uchepechepe unaweza kuathiri ufanyaji kazi wa mota na mapanga ya feni.
Kuna aina mbalimbali tofauti za feni za nje kutegemea na mahitaji na vitu vilivyoambatana na feni hiyo. Kuna ambazo zina taa zilizoshikiliwa humo humo, kuna za rimoti na zenye virekebisho vya ukutani na mwendo wa mpepea. Watengenezaji wa feni za nje pia wanaweka bwembwe za mapanga yanayofanana kama majani. Kwahivyo ukiona feni ya hivyo unajua moja kwa moja kuwa ni ya mazingira ya nje ya nyumba. Pia feni zenye maelezo kuwa zinaweza kuwekwa maeneo ya maji maji ndio zinafaa nje kama kwenye varanda na kadhalika. Feni ya kwenye varanda ikiwa ni ya kuninginia darini na yenye taa humo humo inafaa zaidi.

Mitindo ya feni ipo mingi bila kikomo na baadhi yake imetumika kama mapambo. Kwa mfano kuna mapanga ya feni ya rangi mbalimbali tofauti za kuendana na mapambo yako ya ndani.  Staili mbalimbali za feni zinawezesha kuendana na fenicha zilizopo chumbani. Pia kwa kusisitiza mapambo yako ya ndani unaweza ukachagua nyumba ya mota kwa rangi unayoitaka. Na kama ulikuwa hujui, unaweza kupaka rangi unayoipenda kwenye mapanga na mota kabla ya kufunga feni. Ni rahisi hasa kama mradi wako ni wa kufunga feni nyumba nzima.

Utashangaa ni kwa namna gani feni inaweza kuleta mabadiliko nyumbani kwako, na kama ukiwa na moja kwa kipindi, utapigwa na butwaa ni kwa vipi uliishi bila kuwa nayo.

Makala hii imeandaliwa na Vivi O. Machange. Vivi anajishughulisha na usafi wa mazulia, nguo na magari; pia ana mapenzi makubwa ya mitindo na mapambo ya nyumbani. Kwa maoni au maswali tuma kwenda 0755 200023 au viviobed@yahoo.co.uk

"vitu vizuri"...handbag

hiki kipochi alichobeba mteja wangu fulani ni kizuri. kinavutia bila kuwa na jina tuseme la designer fulani labda wala nini..mradi roho ipende!

wenye majiko kama haya ni watu kama wewe..

 hapa hata kama hujiskii kupika utapika tu. umalize upakue na ukae ule
 hili ni dogo dogo linafaa sana kwa familia changa. vifaa vya kupikia vimepangwa kirahisi hasa vile vya kunyanyua mkono na kuchukua kama mafuta hapo juu na kitufe cha visu.
 hili limenitumbuiza kwani ameweka 'kitu kizuri"...kizulia cha jikoni. mwenyewe hana mchezo ameamua kabisa kuweka kaunta za zege. mambo ya mable hataki..pia feni ya stovu ilee inaning'inia
 hili lina sehemu kubwa ya kufanyia kazi na lina stovu 2
hili rangi rangi zake limekaa ki restaurant zaidi. angalia ubunifu wa kuhifadhi masufuria

Wednesday, October 9, 2013

'''vitu vizuri''...huu unyunyu...

huyu dada ni mteja wangu na mara kwa mara tunakutana ofsini kwangu..ila kwa leo hizi nywele zimenikosha. sikumbuki kuwahi kusuka rasta kichwani  kwangu jamani. du du!!


ameniambia hizi ni rasta za kusuka vitunguu ila mbwembwe ziko kwenye kubana!

mid week stuff

nilipata wakati mgumu (wanasema usiseme shida..ha ha haaa) wakati naanzisha bustani zangu kwa kutaka kujua ni maua/mimea ipi inafaa zaidi kwenye jua na ipi inashamiri kwenye kivuli. nilitembelea bustani mbali mbali za wauza maua na kuwadadisi ma gardener kadhaa. nikafanikiwa na kama wewe ni mmoja wapo mwenye changamoto kama yangu wakati huo wacha nikusaidie upate mawazo. tazama picha hizi hapa chini za maua yanayoshamiri kwenye jua kali kwa maana ya kwamba yanastawi na rangi zake zinakolea zaidi kwenye jua kali. ukiyaotesha kivulini tu yanadoda yanapoteza rangi rangi zake nzuri na yanageuka kuwa kijani. kijani ni kizuri ila kwa wakati huo wewe unachokuwa unataka ni rangi rangi ili kupunguza ukijani kwenye bustani yako.
hili ua nililoshika wanaliita kitenge. yapo ya aina mbili; la kijani na hili la pinki. ukiondoa hili la pinki juani ukaliotesha kivulini linageuka rangi huwezi amini lote linakuwa kijani kwahivyo linafanana na yule ndugu yake. hili la mbele yake lina majani yaliyojisokotasokota. ukiliotesha kivulini nalo mambo ni yaleyale nyekundu yote na njano inapotea
 unaona hayo majani ya njano? ukiyaweka kivulini tu yanageuka kijani


 hili ukiliotesha kivulini linakufa
hiki chekundu hiki ukikiona live utapenda. kina nyekundu nzuri mno na kinapopigwa na jua ndio kinazidi kuwaka

Tuesday, October 8, 2013

morningwood..

ni asubuhi njema na mvua zimetulia kidogo, pia marafiki zangu wa kweli watu wangu wadogo wamefunga shule kwa hivyo mchakamchaka kidogo ume slow down. nipo hapa naangalia uzuri wa asubuhi kijua kinavyochomoza..

Monday, October 7, 2013

nimekuwa bize na kufua gauni la bibi harusi

ian dc tunafua pia nguo za mabibi harusi..karibu sana..leo nilijipinda na hii moja peke yangu kwani ina virembo vingi nikataka kuifanya mwenyewe ili niweke umakini zaidi (usininukuu vibaya kuwa wafanyakazi wangu sio makini...wao ni makini lakini mimi ni makini zaidi..lol) isijeharibika. bei ya kufua nguo kama hii ni 25K tu..hivi wapendwa tunavyoita gauni la bibi harusi shela ni sahihi kweli? je kama gauni ni shela na kile cha kichwani tunakiitaje.

gauni

head piece..je hii si ndio shela na lile ni gauni?? wapi bakita...

rangi hizi zinavutia

nimekuwa napokea ma carpet mengi mengi kwa ajili ya kuyasafisha iwe ni wa kufua ama kunyonya vumbi na mchanga. kati ya rangi za carpets zilizonivutia na ambazo haziko common ni za hizi hapa. sio kama wengi wanavyopenda rangi za brown (nadhani ni ili kuficha uchafu) ama zebra (wanadhani zinaonyesha ufahari fulani) rangi za zulia hili hazifichi uchafu, ni rafiki kwa watoto na zinaendana na vitupio vingi vya mapambo ya ndani..