Mara kadhaa nimeshasikia au kusoma mtu kuangukia kisogo akafa, inasikitisha kwakweli.
MWANAFUNZI wa darasa la tano katika Shule ya Msingi
Ilola, Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Mkoa wa Shinyanga, Veronica Venance (12),
amefariki dunia baada ya kupigwa na mwanafunzi mwenzake wakati wakigombea
daftari darasani.
Tukio hilo limetokea juzi mchana wakati wanafunzi hao
wakiwa darasani wakiendelea na masomo.
Akizungumza na MTANZANIA jana kuhusu tukio hilo, Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Ilola, Mahona Joseph, alidai lilitokea wakati Veronoca
alipong’ang’ania daftari alilokuwa ameazima kwa mwenzake Sophia Mathew (12) kwa
ajili ya kunakili masomo waliyofundishwa.
“Kitendo cha kung’ang’ania daftari hilo wakati si mali
yake kilimkera mwenzake na kuzua ugomvi kati yao, hivyo wakati wakinyang’anyana
ndipo Sophia alipoanza kumshambulia mwenzake kwa kumpiga makofi na ngumi sehemu
za kichwani hali iliyosababishia kifo chake,” alisema Joseph.
Akizungumzia tukio hilo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,
Magere Jonas, alisema kifo cha mwanafunzi huyo kilitokea wakati wakigombana
darasani ambapo kati ya wanafunzi hao mmoja aliangushwa chini na kugonga eneo
la kisogoni.
“Ilikuwa muda wa wanafunzi kupata chakula cha mchana,
ambapo wengine wakiwa bado wapo shuleni na hakukuwa na mwalimu hata mmoja, ila
mimi na mwalimu mkuu msaidizi tulikuwa chini ya mti tunapunga upepo.
“Tukiwa tunaendelea na mazungumzo ghafla alikuja
mwanafunzi mmoja na kutueleza kuna wanafunzi wanagombana darasani, ndipo
tukaenda na kumkuta Veronica amelala chali darasani. Baada ya kuona hali hiyo
tulimchukua na kumkimbiza zahanati ya Ilola ambako walituambia tumpeleke kituo
cha afya Bugisi kwa matibabu zaidi.
“Hata hivyo hali ya mwanafunzi huyo ilizidi kubadilika na
kuwa mbaya na tulipofika Bugisi tukaambiwa tayari ameshafariki dunia, tunahisi
pengine aliumia kichwani,” alisema Mwalimu Jonas.
Kutokana na tukio hilo, MTANZANIA ilimtafuta Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Shinyanga, Longinus Tibishubwamu, ambapo alithibitisha kutokea
kwa kifo hicho.
“Ni kweli kimetokea kifo cha mwanafunzi Veronica. Baada
ya kupata taarifa hizo tulifika katika eno la tukio. Wakati uchunguzi wa suala
hili ukiendelea, Jeshi la Polisi tunamshikilia mwanafunzi Sophia Mathew kwa
mahojiano zaidi.
“Tukio hilo limetokea Februari 24, mwaka huu saa 7 mchana
wakati wanafunzi hao wakiwa darasani kwao wakiendelea na masomo,” alisema
Kamanda
INASIKITISHA SANA AISEE.....POLE KWA WAZAZI
ReplyDeleteSana, halafu wote watoto sidhani huyo mwenzake alifahamu anaweza ua. Itabidi wazazi wasamehe tu.
ReplyDelete