Mfano wa nyumba ya rangi nyekundu |
WAKIMBIZI wanaokimbia vurugu zinazozidi kuongezeka nchini
Burundi wamesema kuwa, wajumbe wa kitengo cha vijana wa chama kinachoongoza
serikali nchini humo wanapaka rangi nyekundu katika nyumba za
watu wanaowindwa, wakala wa wakimbiza wa Umoja wa Mataifa
(UN) umekaririwa mwishoni mwa wiki na Shirika la Habari Uingereza (Reuters) na
kuripotiwa jana.
Kulingana na taarifa jana, pia kuna ripoti za watu
wanaouza mali zao kabla ya kuondoka katika nchi hiyo, hali inayoelekea kwamba
hawategemei usalama wao kwa muda mrefu.
Zaidi ya Warundi 50,000-wengi wao wakiwa wanawake na
watotowamekimbilia nchi jirani katika wiki za karibuni kutokana na vurugu hizo
zilizochochewa na mpango wa Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo kugombea tena
nafasi hiyo kwa mara
ya tatu.
Wapinzani wamekaririwa kuwa, hatua hiyo inakiuka katiba
ya nchi hiyo pamoja na mpango wa amani ambao ulikomesha vita vya kikabila vya
mwaka 2005.
Vurugu hizi zimezuka katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati ambako
hali inasadikiwa kuwa mbaya tangu vita ya miaka 12 ambayo ilizaa waasi kutoka
katika Kabila la Wahutu walio wengi dhidi ya jeshi lililokuwa likiongozwa
na Watutsi ambapo, watu 300,000 waliuawa.
Shuhuda mmoja aliyetajwa kwa jina la Edwards ambaye haikuelezwa
ni nani ameileza Reuters kuwa, wakimbizi waliowasili nchini Rwanda wameelezea
kuhusu manyanyaso na vitisho walivyofanyiwa na wajumbe wa vijana wa
Imbonerakure "ambao wanapaka rangi nyekundu katika nyumba za watu
wanaowindwa."
"Baadhi waliamua kuondoka kama hatua ya tahadhari,
kutokana na kuwahi kukumbana na vurugu za zamani," alinukuliwa akizungumza
jijini Geneva, Uswisi.
Chama kinachoongoza serikali cha CNDD-FDD kimekanusha
madai hayo kuwa, vijana wake wamepewa silaha na wanajaribu kuchochea vurugu.
Kimesema kuwa, wapinzani wao ndiyo wanaojaribu kuongeza msongo.
Edwards alisema kwamba, wakimbizi wanaokimbia wamekuwa
wakikabiliwa na hatari nyingi.
"Baadhi ya wanawake wameripoti vitisho vya kubakwa
kutoka kwa wanaume wenye silaha na wanalazimishwa kutoa hongo ili
waweze kupita katika vizuizi.
Baadhi wametembea kwa saa kadhaa kupitia
porini wakiwa na watoto wao," alinukuliwa.
Wakala wa wakimbizi imesema kuwa, wakimbizi wengi
walitoka Kaskazini ya nchi hiyo, lakini wiki hii ilianza kushuhudia wengine
wakiwasili kutokea mijini ikiwa ni pamoja na shule za juu na wanafunzi wa vyuo
vikuu.
MAJIRA
No comments:
Post a Comment