Wananchi wakiangalia nyumba iliyotekea na kuangamiza familia nzima |
WATU
sita wa familia moja akiwamo Kapteni mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi
(JWTZ), wamekufa papo hapo baada ya kuteketezwa kwa moto jijini Dar es Salaam.
Alisema
wengine waliokufa katika ajali hiyo ni mke wa marehemu, Selina Yegela
anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 50 na 55, ambaye pia ni mstaafu wa
iliyokuwa Kampuni ya Kuhudumia Ndege (DAHACO), sasa Swissport.
Aidha,
moto huo pia umesababisha vifo vya watoto wawili wanaokadiriwa kuwa na umri
kati ya miaka 20 na 30 ambao ni, Lucas Mpira na Samwel Yegela.
Kamanda
Nzuki alisema wajukuu wa marehemu nao wamekufa katika ajali hiyo, ambao ni
Selina Emmanuel (9) mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Minazi
Mirefu na Pauline Emmanuel (3), mwanafunzi wa chekechea katika Shule ya Tumaini
iliyopo Kitunda.
“Chanzo
cha moto huo bado hakijafahamika, tunaendelea na uchunguzi na tunashirikiana na
Shirika la Umeme (Tanesco) ili kubaini chanzo kilichosababisha moto huo,”
alisema Nzuki. Maiti wamehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na
uchunguzi bado unaendelea
No comments:
Post a Comment