Prof anachambua pamoja na mambo mengine , madhaifu ya
Zitto Kabwe na kushauri apatiwe muda wa kujirekebisha aweze kuwa kiongozi wa
kitaifa, mapungufu hayo kwa maneno yake mwenyewe Proffessor:Pengine udhaifu
mkubwa wa Zitto kama kiongozi upo katika maeneo makubwa mawili.
Kwanza, ni
kushindwa kupima maana na matokeo mapana ya kauli zake kabla hajazitoa. Mara
kadhaa Zitto amekuwa akitoa kauli ambazo huacha ukakasi mkubwa katika jamii.
Kwa mfano, akiwa katika kampeni za ubunge mwaka 2010
alitangaza kwamba katika awamu ijayo angerudi kugombea urais na siyo ubunge
tena.
Zitto alitoa tangazo hili huku akijua kwamba chama chake
kilikuwa na mgombea urais na kwamba kauli kama ile ingeweza kupunguza imani ya
wapiga kura kwa mgombea wa chama chake kwa kuonyesha kwamba asingeshinda na
pengine alikuwa hafai.
Pili, baadhi ya kauli za Zitto huonyesha kwamba ni
kiongozi anayechokozeka kirahisi.
Kwa mfano, alipomwagiwa ‘upupu’ na Tundu Lissu mapema
mwaka huu kwamba alikuwa amehongwa magari na Nimrod Mkono, Zitto alitoa kauli
ya haraka tata kwamba, yeye asingekufa kama alivyokufa Chacha Wangwe (“Chacha
died, I won’t”).
Hii ni kauli tata kwa sababu inatoa taswira kwamba
pengine Chacha Wangwe hakufa kwa ajali kama inavyojulikana bali aliuawa na watu
ndani ya chama chake.
Pili, kwamba yeye asingekufa kama Wangwe inaweza kutoa
taswira kwamba Zitto ana nguvu za ziada za kumkinga na kifo.
Eneo la pili la udhaifu wa Zitto lipo katika mahusiano ya
kimapenzi yasiyoeleweka kwa mtu mwenye dhamana ya uongozi. Zitto amekuwa
akihusishwa na wasichana kadhaa maarufu hapa nchini ambao maadili yao kindoa
yanatia shaka katika mazingira ya Kitanzania.
Inapokuja katika mahusiano ya kimapenzi, Zitto hujisahau
kabisa kwamba yeye ni kiongozi mkubwa katika jamii pamoja na kwamba ana haki
zake kama binadamu.
Pengine hili ndilo eneo ambalo Zitto ameshindwa
kujitofautisha na wanasiasa wenzake hapa nchini, ambao wengi wao nao uadilifu
wao katika eneo hili ni wa mashaka.
VIJIMAMBO
No comments:
Post a Comment