Staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja anaendelea vizuri
baada yakupigwa chupa na kijana mmoja usiku ya kuamkia jana wakiwa kwenye show
ya mwanamziki Mabeste aliyoiandaa ili kuchangisha pesa kwa ajili ajili ya
matibabu ya Mkeo.
Akilezea tukio hilo la kupigwa na chupa hapo jana
alipofanya mahojiano na mtangazaji Millard Ayo wa Clouds FM kajala alieleza
“Mpaka tumemaliza show, sasa kwenye muda wa kuondoka
nikamwambia Meneja wangu amuite msanii wetu mmoja anaitwa Tausi ili tuondoke,
sasa wakati nataka kushuka kwenye gari natembea tu sijui chochote nikashangaa
chupa imenipiga usoni, nikadondoka na kubiringita kwenye zile ngazi, kuna mkaka
na mdada wakaniona wakanisaidia”
Akaongeza kuwa;
“Aliyenipiga na
hiyo chupa ni Mwanaume, simjui na wala sijawahi kumuona hata mara moja….
amekamatwa yuko Osterbay Polisi, nilivyotoka Maisha Club nilipelekwa Hospitali
Mwananyamala nimeshonwa usoni aliponiumiza, tukarudi Polisi nikaandika
maelezo”.
Pole sana Kajala
BONGOMOVIES
No comments:
Post a Comment