Bila
shaka unaponunua jokofu, unategemea lifanye kazi vizuri kwa miaka mingi ijayo.
Hata hivyo ili jokofu lako liweze kutimiza matarajio hayo, hupaswi kuliacha tu
bila utunzaji. Njia sahii za utunzaji
zitasaidia kifaa hiki kufanya kazi bila matatizo na kwa muda mrefu. Tupate
ujuzi ufuatao
toka kwa mtalam wa majokofu bwana Hafiz Ali kama ifuatavyo:
Lipe nafasi za
kupumua
Jokufu
lako linahitaji nafasi za kutolea hewa ili liweze kufanya kazi vizuri. Kama
umeweka jokofu likakabana moja kwa moja na ukuta lazima lifanye kazi ya ziada
kuweka vyakula vyako baridi, ambapo halikutengenezwa kufanya kazi hiyo ya
nyongeza. Wakati unapochagua mahali pa kuweka jokofu hakikisha angalau kuna
nafasi wazi ya inchi mbili kila upande. Hii kwa upande wa nje na ni la
kuzingatia sana hasa yale majiko ambayo yameshajengewa tayari eneo la kuwekea
jokofu. Kwa upande wa ndani hakikisha kuwa hauhifadhi humo vyakula kwa mtindo
wa vitu vikubwa na vilivyoshikana bila kuachiana nafasi.
Safisha koili za
nje
Ni
bahati mbaya kuwa pamoja na walio wengi kusafisha majokofu yao vizuri sana kwa
ndani na milango kwa nje, wengi wetu tunasahau nyuma ya jokofu. Ambapo ndio
kuna zile koili zinazosaidia kufanya chakula kibaki na ubaridi kwa sababu koili
hizi zinaondoa joto toka ndani ya jokofu na friza. Kutegemea na muundo wa
jokofu zipo koili zilizo nyuma au chini na ni rahisi kwa vumbi na chembechembe
za uchafu kujishika humo baada ya muda.
Uchafu huu unasababisha jokofu kuongeza msukomo wa kazi yake ambapo inapelekea
kulichosha na kusababisha matengenezo ya gharama.
Uzuri
ni kwamba kusafisha koili za nje ya
jokofu ni hatua rahisi ya utunzaji wake ambayo unaweza tu kuifanya wewe
mwenyewe. Zima jokofu, livute mbali na ukuta na tumia ufagilio wenye brashi
laini kusafisha. Mavumbi yote yatadondoka sakafuni ambapo utasafisha sakafu baadaye.
Fanya hivi kila baada ya miezi 6 kusaidia jokofu lako kufanya kazi vizuri.
Mipira ya
milangoni iwe inakaba
Ili
jokofu liweze kufanya kazi vizuri na pia matumizi mazuri ya nishati, milango
yake inatakiwa iwe inabana kabisa. Milangoni mwa jokofu kuna mpira ambayo huwa
unakuwa dhaifu baada ya muda. Inapotokea hivyo hewa ya nje ambayo ina joto inapenya
na kuingia ndani ya jokofu, na kulisababishia kufanya kazi ya nyongeza kuondoa
hilo joto la ziada. Hii inamaanisha bili kubwa za umeme na pia jokofu kuchakaa
mapema.
Kuisaidia
mipira ya milangoni idumu, uwe unaisafisha baada ya kipindi kwa sabuni na maji.
Kama unahisi imeanza kudhoofika fanya jaribio jepesi: Kungua mlango uufikishe
nusu halafu uachie polepole ujifunge wenzewe. Kama haubani vizuri basi tayari
mpira umeanza kuchoka. Habari njema ni kwamba mipira ya spea ipo na sio bei
kubwa na vilevile kuibandika upya ni rahisi tu.
Liyeyushe kila
baada ya kipindi
Kama
jokofu lako ni moja ya matoleo mapya utakuwa una bahati kwamba halijengi barafu
ndani (non frost) na huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu dondoo hii ya
utunzaji. Ila kama ni la zamani kidogo, bila shaka una hii kadhia ya barafu
kujaa ndani.
Barafu
zinazojitenga katika koili zilizo ndani ya jokofu zinalilazimisha kufanya kazi
ya nyongeza ili kubaki katika ubaridi unaotakiwa.
Barafu
inapojijenga hadi inchi moja na nusu ni wakati wa kuyeyusha jokofu. Zima umeme,
ondoa vyakula vyote, acha milango wazi na acha kifaa kiyeyuke. Endapo hujalitoa
nje ya nyumba, unaweza kubeba mabonge ya barafu kadiri yanavyojiachia na kuweka
kwenye chombo ili kuepuka maji wengi kujaa ndani. Mara barafu yote inapoyeyka,
mwaga na kausha mashelfu yaliyojikusanya maji, washa jokofu na rudishia vyakula
vyako.
Nifuate instagram @ vivimachange
No comments:
Post a Comment