Monday, April 18, 2016

Vitu 7 ambavyo kila chumba cha kulala kinavihitaji

Chumba kilichokamilika kina kuta, mlango, dari na dirisha. Kwenye makala hii tunaangalia vitu vinavyohitajika ndani ya chumba kamili cha kulala.
Chumba chako cha kulala ndio sehemu yako takatifu, je kwanini
usihakikishe kina vitu hivi?

1.      Kitanda na matandiko
Kimsingi vitu hivi ndivyo vimefanya chumba hiki kiitwe ni cha kulala.

2.      Zulia
Hakuna sakafu inayoweza kuburudisha miguu peku unapotoka kuamka asubuhi kuliko ya zulia. Jipendelee kwa kuhakikisha kuwa hatua yako ya mwanzo wa siku ni ya burudani. Hata kama huwezi kununua zulia la kutosha chumba kizima basi weka japo dogo la pembeni kwa kitanda.

3.      Mito ya kutosha
Kulingana na ukubwa wa kitanda chako, idadi sahihi ya mito ni miwili hadi sita. Kitanda kiwe na mito ya kulalia pamoja na ile ya mapambo. Na pia muundo  wa mito ya mapambo waweza kuwa wowote kama vile pembe nne, soseji na moyo. Kwa kulalia, mito inayofaa zaidi ni ya pembe nne.

4.      Eneo la kukaa (ambalo sio kitandani)
Eneo la kukaa linakusaidia wakati wa kusoma au wa mazungumzo na mwenzi wako. Pia ni pazuri kunyanyulia mguu wakati wa kuvaa soksi. Vilevile unapotandua matandiko kwa ajili ya kulala unahitaji  kuondoa na kihifadhi vile vitu ulivyopambia kitanda kama vile mito, utepe wa kitanda na shuka au duveti la mapambo. Ingawa kwa baridi inabidi utumie huu uzinduzi wa Ulaya (duveti) kujifunikia. Eneo la kukalia kwenye chumba cha kulala linakusaidia kuhifadhi vitu hivi (kwa ajili ya kuvitandika kesho yake) badala ya kuviweka chini.

5.      Sanaa na picha unayoipenda
Haimaanishi kwamba chumba kiwe na mrundikano wa picha na sanaa ila unapoweka vitu vichache unavyovipenda eneo unaloviona kwa muda mrefu ni kwamba inazidisha furaha yako. Unapokuwa na furaha unapata usingizi mzuri na unaanza siku kwa furaha.

6.      Taa za vivuli kila upande wa kitanda
Kuna wakati ukiwa umelala unajisikia kusoma kitabu, jarida au gazeti. Ili usimsumbue wa pembeni yako kwa mwanga asiohitaji, kutumia taa ya kivuli iliyo upande wako ndio suluhisho. Zaidi ni kwamba taa hizi ni sehemu ya kupendezesha chumba.

7.      Pazia
Chumba cha kulala si kama cha jikoni. Kinahitaji faragha na hisia za giza hata kiwe ni cha rangi za mwanga kiasi gani. Weka pazia sahihi.

Namaliazia kwa kukuuliza swali msomaji wangu, je chumba chako kina vingapi kati ya hivi?

Makala hii imeandaliwa na Vivi ili kukuelimisha kupendezesha nyumba yako. Simu 0755 200023 

No comments:

Post a Comment