Monday, March 27, 2017

Uhusiano kati ya saizi ya marumaru za sakafuni na ukubwa wa chumba



Kwa kawaida hakuna chumba ndani ya nyumba ambacho unaweza ukasema kuwa hakifai kuwekwa sakafu ya marumaru, cha muhimu ni kuchagua saizi sahihi kwa mahali unapotaka kuweka.

Bwana Hamid 0776 756 197 wa duka la kuuza marumaru la SS Tiles lililopo makutano ya mtaa wa Swahili na Narung'ombeKariakoo anasema kuwa
marumaru za sakafuni zinakuja kwa ukubwa mbalimbali kuanzia ndogo kabisa hadi kubwa kabisa. Zipo za mraba kuanzia sentimita 20 kwa 20 hadi 120 kwa 120 na pia za mstatili kuanzia sentimita 10 kwa 60 hadi 120 kwa 180 na wakati huo huo bila kusahau za kuwekwa kimshazari.

Unaweza ukazitumia kwa manufaa ya kufanya chumba kionekane kikubwa au kipana kama utachagua za ukubwa na umbo sahihi.
Kwa maana hiyo ni vyema kuchukua muda kutathmini chumba au sakafu unapotaka kuweka marumaru na kufuata dondoo zifuatazo wakati wa kuamua ukubwa wa marumaru hizo.

·        Marumaru za saizi kubwa zinaweza kufanya chumba kidogo kuonekana kikubwa.

Kimuonekano, chumba kidogo kinaweza kuonekana kikubwa pale kinapokuwa na sakafu yenye marumaru kubwa. Wakati ukizingatia dondoo hii inakubidi, ufahamu uwiano wa marumaru kuendana na ukubwa wa chumba. Kwa mfano kama marumaru hizo ni kubwa na kwamba inatahitajika fundi kuzikatakata sana basi hazitakuwa na muonekano wa kuvutia. Lakini chumba ambacho kwa ukubwa wake inawezekana kuweka marumaru kubwa na zote zikafiti bila kukatakata basi hakika kinapendeza.

Pia kama chumba kinachowekwa marumaru za sakafu kitawekwa pia za ukutani, kwa mfano jikoni au bafuni inashauriwa  marumaru za ukutani zisiwe za saizi kubwa kuliko zile za sakafuni.

·        Marumaru kubwa ni imara zaidi

Unene wa marmaru kubwa ni mpana kuliko wa marumaru ndogo. Kutokana na dondoo hii kwamba marumaru kubwa ni imara zinafaa kuwekwa kwenye vyumba vikubwa kama vile sebuleni na hata kwenye ujia kwa ajili ni maeneo yanayokanyagwa zaidi.

·        Ziwe kubwa au ndogo ni chaguo lako!

Ingawa ni imani ya kawaida kuwa marumaru za maumbo madogo zinafaa kwa chumba kidogo wakati zile kubwa ni kwa vyumba vikubwa, kiukweli ni swala la maamuzi binafsi na sababu za kiufundi. Kwa mfano mtu anayependa muonekano wa kisasa atafurahia marumaru za kuanzia ukubwa wa sentimita 45 kwa 45, iwe vyumba ni vikubwa au vidogo. Cha muhimu ni fundi akuhakikishie kuwa hakatakuwa na kuzikatakata sana. Wakati wale wanaopenda mitindo ya kizamani watapendelea zile ndogo ndogo.

Pia wapo wanaopendelea kuchanganya marumaru za saizi tofauti tofauti. Nyumba ni yako chaguo ni lako!
 Endapo uko kwenye ujenzi na unahitaji marumaru za uhakika muone Hamidu mtaa wa Swahili na Narung'ombe Kariakoo. Ukienda kwa code VIVI unapata punguzo hadi asilimia 30.

No comments:

Post a Comment