Ingawaje wenye nyumba wengi pamoja na wenye nyumba
watarajiwa walionekana kutofuatilia sakafu za mbao kwa sababu tu ni gharama
kuliko aina nyingine za sakafu kama vile marumaru na zulia, kwa siku za
karibuni kumekuwepo na mwamko wa watu hawa kuanza tena kujenga upendeleo wa
kuwa na sakafu za mbao. Ni kweli kuwa pamoja na kwamba utaongeza gharama kidogo
ni kuwa kuna faida nyingi za kuwa na sakafu ya mbao. Karibu tuangalie baadhi ya
faida hizi kama zinavyoelezwa na fundi wa sakafu hizi bwana Andrew Komba:
1. Sakafu ya mbao yenye ubora inadumu kwa miaka angalau 15 kabla ya
kufanyiwa ukarabati. Wakati watu wengi wanajikuta wakibadilisha zulia kila
baada ya miaka mitano, kutokana na madoa, matundu au
tu manyoya kuisha baadhi
ya maeneo kutokana na uchakavu, utagundua kuwa sakafu ya mbao inazidi kupendeza
kadri miaka inavyosogea.
2. Ni rahisi kusafisha sakafu ya mbao kuliko ya zulia. Sababu ziko wazi,
ufagio tu au dekio la juu juu linafanya sakafu ya mbao ing’ae. Kama watoto
wameingiza tope ndani dekio lililoloa kidogo tu linamaliza tatizo kirahisi
kabisa. Wenye sakafu za zulia wakati kama huu wangekuwa wakipiga yowe. Ingawa
vilevile ni rahisi kusafisha sakafu ya marumaru ila kiusalama wakati ikiwa
imeloa ina nafasi kubwa ya kuangusha watu hasa watoto na watu wa umri mkubwa.
Na pia bila kujulishwa si rahisi kuona eneo lililoloa. Na kwa swala la matope
halipatana kabisa na bidhaa inayounganisha marumaru moja na nyingine yaani
grauti.
3. Sakafu ya mbao ni salama zaidi kiafaya kuliko zulia. Kuna ripoti nyingi
za kuogofya kuwa mazulia yamekuwa yakihifadhi vijidudu na vumbi ambapo
husababisha mzio hasa kwa watoto wadogo ambao muda mwingi wanakuwa wamekaa
chini. Hii pia inahusika kwa nyumba zenye sakafu la zulia huku zikiwa na mbwa
au paka ndani.
4. Sio tu kwamba sakafu ya mbao ni salama zaidi kiafya bali pia hazidaki
harufu mbaya kutoka kwa wanyama wa ndani au kivimiminika na vyakula ambayo
vimemwagikia. Harufu ya sakafu ya mbao ni freshi na mng’ao wa polishi unafanya
nyumba kuwa na mvuto.
5. Kama isivyo kwa sakafu ya marumaru sakafu ya mbao haina ubaridi na wala
huna haja ya kupasha joto miguu kwa kuvaa soksi kama vile ambayo ingekuwa
kwenye marumaru hasa nyakati na maeneo ya baridi.
6. Kama baada ya miaka kadhaa sakafu ya mbao itakuwa na mikwaruzo aidha kutokana
na kusogeza vitu au tuu uchakavu wa kawaida, kuita fundi na kujaza kemikali ya
sand and seal pamoja na kupaka polishi inairudisha kwenye upya tena. Hii ni
gharama nafuu zaidi kuliko kutandaza zulia jipya.
7. Moja ya faida kuu ambayo watu wanaisahau au hawaijui kuhusu sakafu ya
mbao ni ile hali ya kutopitwa na wakati. Mazulia na marumaru yanakuja kwa mitindo
mipya kila leo lakini sii kwa sakafu ya mbao. Mbao zimedumu karne na karne na
kila siku zinaongezeka thamani na umaarufu.
8. Ingawaje kale ilionekana kama sakafu ya mbao ni kwa ajili ya nyumba za
“wenye nazo”, teknolojia imewezesha njia za uzalishaji ambapo inawezekana
kumudu sakafu ya mbao kwa bajeti tofauti tofauti.
9. Wadau wa nyumba kama vile wajenzi, madalali, wenye nyumba na wapangaji
wote wamekiri kuwa nyumba yenye sakafu ya mbao ina thamani mara mbili iwe ni
kwa kuuza au kupangisha kuliko nyumba zenye aina nyingine za sakafu.
Kwahivyo ingawa inaweza kukugharimu gharama kidogo
zaidi, ila kwa suluhisho la muda mrefu sakafu ya mbao ni bora zaidi. Kutokana
na faida hizi 9 fikiria mara mbili kabla ya kufanya uamuzi wa sakafu unayotaka
kuweka. Muulize mwenye nyumba yeyote aliyeweka sakafu ya mbao na atakuambia
kuwa ni uamuzi mzuri aliowahi kufanya kwenye maisha yake!!
Kwa mahitaji ya sakafu za mbao tuwasiliane 0755200023
No comments:
Post a Comment