Kutokana
na uwepo wa vyandarua vya maumbo na uwekaji wa aina nyingi inaweza
kukuchanganya kwamba ni kipi sahihi kwako.Usihamaki! Hapa nitakupa muongozo wa
kile unachotakiwa kufahamu kwa baadhi ya maumbo maarufu zaidi ya vyandarua vya
kisasa sokoni.
Naamini
muongozo huu utakusaidia kuchagua chandarua sahihi ili usiendelee kutafunwa na
mbu ukiwa bado hai! Kama unachanganyikiwa na vyandarua vya umbo la
kengele,
boksi, vya kuchimbia darini au ukutani au hata vyenye eneo moja la kuingilia au
maeneo manne au hakijapasuliwa kabisa na kadhalika karibu ujielimishe
Vyandarua vya kujitegemea
Vyandarua vya kujitegemea ni aina ya nyandarua ambavyo vina fremu zake ambazo
aidha ni bomba za chuma, plastiki au aluminiam ambapo vinashikilia godoro na neti kama
vile hema. Havihitaji sehemu yoyote ya kuning’inizwa na vina zipu kiasi kwamba
mlalaji ukiwa umelala unakuwa umejifungia kabisa ndani.
Faida za
vyandarua vya muundo huu ni uwekaji wake ambao ni rahisi, huhitaji ngazi, kulabu
, kutoboa wala fundi. Vinaweza kutumika popote ndani kitandani au varandani
sakafuni. Mazingira yake ya ndani ni salama zaidi kwa watoto wadogo n wachanga,
kinasaidia kumkinga asianguke hata pale anapojigeuza.
Changamoto
yake ni kwamba kwa ajili vina fremu za kukishikilia vinachukua nafasi hasa pale
unapotaka kusafiri nacho mbali tofauti na vile vya kutundika darini visivyokuwa
na fremu. Mabomba yake hayajikunji kirahisi.Fremu yake ikiharibika inaweza kuwa
changamoto kuifanyia marekebisho. Vinafaa zaidi kwenye vitanda vidogo kwani
hata utandikaji unakuwa rahisi kwa ajili kumbuka kuwa godoro linaingizwa ndani
ya chandarua. Huwezi kuketi kitandani wakati wa mchana kwa kuning’iniza miguu.
Vyandarua
vya umbo la kengele
Hivi ni vile vyandarua vyenye umbo kama
la kengele. Ni vya kale zaidi ambapo vina pointi moja tu ya kutundika kwa
kulabu ya darini. Eneo la juu ni jembamba na chandarua kinatanuka kadri
kinavyofikia matandiko. Faida ya vyandarua hivi ni kwamba ni gharama nafuu. Ni
rahisi kukiweka na kukiondoa hasa wakati unapohitaji kukifua. Ni rahisi
kufungasha wakati unapotaka kusafiri nacho. Vinaweza kutumiwa kwenye vitanda
mbalimbali kuanzia vile vidogo vya watoto wanaosoma shule za kulala, vitanda
vya hosteli na vikubwa vya nyumbani.
Changamoto yake ni kwamba vingi ni
vyembamba ambapo kuchomekwa na uchomolewa kila wakati vinakifanye kiwe rahisi
kuchanika. Inahitajika kuwe na kulabu na dari imara.
Vyandarua vya umbo la boksi
Vyandarua hivi ni vya kisasa zaidi.
Vina umbo la boksi ambapo vinafiti kwenye kitanda chote na vinasimikwa aidha
kweye kona za kitanda, ukutani au darini kwa pembe zote nne. Vina bomba zake
maalum za kutengeneza huonekano huo wa umbo la boksi. Huwa vina urembo wa
kuzunguka chandarua na hivyo vinakuwa ni kama pambo chumbani. Vinatakiwa
kutumika ndani ya nyumba na kwa sehemu ya kudumu kama vile chumba cha kulala,
hospitalini au hotelini. Vipo vyenye kamba ya kukifungua na kufunga na kupitia
reli za fremu au kwa staili ya kupandika na kushusha.
Faida za vyandua vya boksi ni uhuru
wake katika matumizi ambapo vina nafasi kubwa kuliko vingine vyote.
Changamoto zake ni kwamba huwezi
kukifunga mwenyewe, ni lazima umhusishe fundi. Vilevile ni ngumu kukifungua
unapotaka kukifua kama hujaonyeshwa na fundi namna ya kukitoa. Hii ni kwasababu
kimeuganishawa kwenye maeneo mengi kutokana na fremu na ukubwa wa chandarua
hiki. Watoto wanapenda kuvuta kamba zake wakati ambapo hakitumiki. Kumbka
kuziweka kwa juu zisining’inie ili wasiweze kuchezea.
Msomaji wangu, ni vyema kufahamu
ukubwa wa mahali unapotaka kuweka chandarua kwani feni au taa darini vinaweza
kuleta kikwazo. Nina hakika umepata mwanga kuhusiana na aina mbalimbali za
vyandara zilizopo sokoni.
Kwa
mahitaji ya neti toa oda yako 0755 200023.
No comments:
Post a Comment