Thursday, July 20, 2023

WANANDOA PRINCE HARRY NA MEGHAN MARKLE WANADAIWA KUTENGA MUDA KUISHI KILA MMOJA KIVYAKE

Ripoti mpya kutoka mtandao wa #RadarOnline inadai kuwa wanandoa #PrinceHarry na mkewe #MeghanMarkle wamejipa likizo kila mmoja anaishi kivyake kwa sasa wakijitafakari ni hatua ipi ifuate katika ndoa yao baada ya misukosuko iliyotokana na madili yao kufeli.

Msongo wa mawazo kati yao unaripotiwa kuanza baada ya kukosa dili la $ milioni 20 spotify na podcast yao Archetypes kushindwa kupata msimu wa pili, chanzo kimesema.

Vyanzo kutoka familia ya kifalme vinaamini Harry anajaribu 'kujitafuta'  baada ya mabadiliko mengi toka aondoke kwenye kasri.
"Wanajitahidi kujitafakari ni nini kimewagonga', chanzo kimefunguka.
" Harry hafiti kwenye mishe za ulimwengu wa Meghan."

Aidha vyanzo hivyo vimeuambia mtandao wa Radar kuwa Harry ana tripu ya kwenda Afrika kufilimu dokumentari yake ya Netflix kwahivyo vinaamini safari hiyo itamuonyesha picha ya hatua inayofuata kwenye ndoa yake.

Safari hiyo ya Harry pekee inatarajiwa inaweza kuwa ndio kitu Harry anahitaji kwa ajili analichukulia bara hilo kama "nyumbani kwake kwa pili na mahali ambapo anajisikia zaidi kuwa yeye", chanzo kimesema.

" Kutawanyika kila mmoja bara tofauti inatarajiwa kuwasaidia kuona ni namna gani wasonge mbele."

Wakati huohuo vyanzo vimesema Meghan tayari ana wakala bomba kwa kum brandi, "anataka ajirandi yeye kama yeye atengeneza mamilioni", mtaalam wa maswala ya kifalme Daniela Elser amesema. "Ni kwa mara ya kwanza kila mmoja anajijenga kitaaluma kwa njia yake."

" Meghan na Harry wapo kwenye presha kubwa kifedha ili kuishi maisha ya kifahari ya California ikiwa ni pamoja na jumba lao la dola milioni 14 pamoja na ulinzi wa hali ya juu", chanzo kimesema.

Ndoa ya miaka mitano ya Prince Harry na Meghan Markle imepitia kashkashi nyingi zikiwemo baadhi ya media kubwa za Uingereza kuwakeka kwenye picha hasi, kuhamia California na kuachana na majukumu ya kifalme na kufunguka kwa kina hadharani mambo hasi waliyopitia kama wanandoa kwenye familia ya kifalme.




Nifollow instagram @vivimachangeblog

Kutangaza Biashara yako hapa wasiliana 0755200023


No comments:

Post a Comment