Monday, July 10, 2023

BARNABA NA RAYA WAMEFUNGA NDOA

Mwanamuziki wa bongo fleva Barnaba na mpenzi wake wa muda mrefu Raya wamefunga ndoa.

Barnaba ambaye alibadili dini kufuata ya Raya sasa anaitwa Mohamed.

Kamati imezawadia shilingi milioni 2.

Raya mjasiriamali wa saluni ya kike ni mtoto wa muigizaji machachari Mama Kimbo.

Mama Kimbo akitoa nasaha zake amesema amefurahi sasa kuwa mkwe halali.

Kwa hadharani hii ni ndoa ya mara ya pili kwa Barnaba ambapo awali alimuoa mrembo Zuu Namela ndoa ambayo baadaye ilivunjika.

Barnaba na Zuu wamejaliwa mtoto mmoja anayeitwa Steve.

Barnaba na ex wake Zuuh wana mahusiano mazuri na wanashirikiana malezi ya Steve ambapo Raya naye mara nyingi anashea mitandaoni akiwa na mtoto wake wa faida Steve.

Nifollow instagram @ViviMachangeBlog

Kwa huduma ya Matangazo wasiliana nami namba 0755200023

No comments:

Post a Comment