sehemu nyingi za bustani za wauza maua kwa mfano pale mapambano sinza, hapo kijito na pale kawe utapata maua na mimea ya kufaa kuotesha kwenye vyungu vya ndani. kwa kuwa sio kila ua au mmea unaofaa kuoteshwa kwenye vyungu kwani inategemea mizizi ya mmea, kiasi cha jua a maji kinachohitajika kwa mmea husika. mimea ya kuotesha kwenye vyungu ikiwa na mizizi mikubwa na inayoenda mbali inapasua chungu kwa ajili inataka kutokeza isambae zaidi.
|
mmea huu ni jamii ya aloe vera ambao nadhani hakuna mtu ambaye hajasikia jina hili kwani vipodozi lukuki na virutubisho kibao vimewekwa aloe vera |
|
hii ni jamii ya magimbi ambayo majani yake yana mistari iliyokolea. huwa inapendezesha sana ndani na baadhi ya watu wanakuwa wabunifu kwa kuongeza uzuri wa muonekano wa majani yake kwa kuyapaka mafuta kidogo, yanakuwa yanang'aa vizuri. |
|
magimbi ambayo mistari yake ya kwenye majani haionyeshi |
No comments:
Post a Comment