sio siri ninapenda makazi mazuri yenye kazi za mawe na huwa nikiyaona nayachungaza kwa undani na kutafakari kwa kina. ninafurahia kuona vitu vimejengwa vizuri kwani huwa naamini mwenye hiyo nyumba anakuwa amefanikiwa kuifanya ndoto yake kuwa kweli kwa kuweza kupata mafundi waliomfanyia kazi ambayo hata mimi mpita njia nikiiona naifurahia. leo nimeamua ku blog kazi za mawe ambazo zinaifanya nyumba iwe sehemu imara.
mawe ya kukanyagia ambayo yanasaidia kuunganisha bustani na sehemu nyingine za nyumba |
vitofali vya chini (paving blocks) ambavyo fundi anaweza kukutengenezea kwa umbo unalotaka na pia unaweza kuweka rangi kama kijani au nyekundu |
ukuta uliowekwa mawe ya Tanga ambayo yaweza kuwekwa hata sakafuni pia |
mawe ya sakafuni ambayo yametenganishwa kwa changarawe.buni kadri uwezavyo, wanasema sky is the limit |
ukuta mfupi wa mawe. wafaa hasa kwa wale wenye makazi ya karibia na bahari |
haya yamewekwa ili kutengeneza njia ya miguu |
No comments:
Post a Comment