Seli za mbegu za kiume zimetengezwa katika maabara kwa
mara ya kwanza na hivyobasi kuwapa matumaini wanaume wasio na uwezo wa kupata
watoto.
Kampuni moja nchini Ufaransa imedai kwamba imefanikiwa
kubadilisha vipande tofauti vya maumbile hadi kupata mbegu za kiume zinazoweza
kutoa mtoto kwa mara ya kwanza.
Iwapo uzinduzi huo utathibitishwa ,huenda ukabadilisha
maisha ya wanaume wengi duniani ambao hawawezi kutoa mbegu za kiume.
Maabara ya Kallistem,kituo cha kibinafsi cha utafiti
kilichopo mjini Lyon kimesema kuwa kitaweza kufanya majaribio katika kipindi
cha miaka miwili.
Iwapo uzinduzi huo utaingia sokoni,kampuni hiyo inataraji
kuwatibu watu 50,000 kila mwaka soko ambalo linaweza kuwa na thamani ya pauni
bilioni 1.7 .
Hatahivyo matokeo ya utafiti huo hayajachapishwa ama hata
kuthibitishwa huku wataalam wa Uingereza wakichukulia uvumbuzi huo kama uvumi
tu.
Kalliste imesema kuwa imefanikiwa kubadilisha seli za
kawaida katika mbegu za kiume hadi mbegu za kiume zilizokomaa.
BBC
No comments:
Post a Comment