Njia 3 za kufanya kuwa mahusiano mazuri
zaidi
Mimi sio expati
wa mahusiano. Ila nimegundua kuwa japo kila mahusiano ni ya kipekee na yanatofautiana
ya kati ya mtu na mtu kuna vitu vitatu
ambavyo mahusiano yoyote yakivifuata vitaboresha uhusiano wa mtu na mwenzie. Nakualika kujua hivi vitu vitatu tu: Kuwa
mkweli. Kuwa tayari kukubaliana kutokubaliana . Kuwa tayari kukimbia.
Kuwa mkweli
Kutokuwa mkweli katika mahusiano ni sumu. Ni ngumu sana kukumbuka uongo wote uliowahi sema na ni nani ulimwambia. Kudanyanywa kunaumiza, Kuna faida nyingi ukiwa mkweli kwa patna wako. Kuna uhuru unaokuwa ndani yake na ulinzi wa kujiamaini kuwa unaambiwa ukweli daima.
Kuwa tayari kukubali kutokubaliana
Inapokuwa ulikuwa singo kwa muda, una maono fulani kichwani kwako juu ya mambo fulani kuwa ndivyo unavyotaka yawe. Mara anakuja huyu mtu ambaye umempenda lakini ana mawazo tofauti na yako kwa labda kila unachotaka. Unajikuta inabidi ulegeze msimamo wako kiasi. Na unaona ni sawa tu. Lakini vinakuja vile vitu ambavyo unajisikia kabisa lazma viwe hivi na sio vile, unatakiwa kuwa na uhakika kuwa patna wako amekubaliana na wewe. Kwa hiyo ukiweza kulegeza msimamo kidogo na kuweka wazi kwa patna wako mnaweza kuja na solution ambayo itakuwa bora zaidi na wote mkaifurahia.
Kuwa tayari kukimbia
Fuata moyo wako. Unajua wakati mambo hayaendi sawa au jambo fulani patna wako alilofanya halileti heshima kwako. Ujue nini, unatakiwa ujipe raha mwenyewe. Kama unahisi kuwa hufurahii mahusiano yako ni sawa kukimbia hata kama ni kwa muda ili utulize kichwa uamue ni nini hasa unataka. Usijali watu watasema nini: chukua maisha yako mikononi mwako. Saa nyingine kujiondoa kwenye uhusiano ni kitu chema zaidi unachoweza kufanya kwako na kwa huyo mtu mwingine.

No comments:
Post a Comment