Taa za mezani ni muhimu kwa kila chumba si tu kwa ajili ya mwanga bali pia ni moja ya pambo la kuongeza
rangi na staili. Kuzinunua inabidi kuwa makini ili usipoteze hela yako na muda
vile vile. Hapa nimekuandalia dondoo unazopaswa kuzingatia wakati wa kufanya
manunuzi.
Fahamu kazi ya taa ya mezani unayotaka
kununua. Je, ni kwa ajili ya kusomea au
ni pambo tu au ni kwa ajili ya wakati wa burudani? Ukishajua
lengo lako la kununua taa hiyo itakusadia kufahamu vitu vya kuzingatia kama
vile ukubwa, rangi ya kivuli chake na aina ya balbu inayotakiwa.
Meza utakayoweka taa yako ikoje? Kuweka juu ya
meza fupi na isiyo imara sana (kwa mfano meza ya kioo chembamba) unapaswa kununua
taa nyepesi na yenye mlingoti mwembamba. Vilevile taa ya kuweka kwenye meza
ndefu inafaa iwe fupi na yenye mlingoti mnene.
Kwa upande wa balbu kama taa ni kwa ajili ya
mapambo unatakiwa ununue balbu ya mwanga hafifu, na kama ni ya kusomea ni
kinyume chake ili kuleta mwanga mwingi. Mara zote weka balbu ya kuendana na
lengo la taa yako.
Nunua taa za mezani kwa kuzingatia mapambo
mengine ya ndani mwako ili kuleta mandari yenye uwiano.
Taa za mezani si bei ndogo kwa uchumi wa sasa,
kwahivyo hakikisha unafanya manunuzi sahihi na nunua kwenye duka la kuaminika
ubora wa vifaa vyake. Ili taa yako iwe na muonekano wa upya kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment