Hebu jiulize kidogo kama mgeni akikutembelea bila taarifa
unajisikia aibu kwa jinsi nyumba ilivyo. Kama ndiyo basi inaonekana una nyumba
isiyokuwa safi kila wakati.
Fikiria ni kwa jinsi gani zaidi ungeweza kuwa
na maisha ya raha kama ya watu wenye nyumba ambazo inachukua dakika 15 tu
kuweka kila kitu sawa na hivyo nyumba yote kuonekana nadhifu.
Nimetafiti tabia za kila siku za watu wenye nyumba safi
– zingatia neno “tabia.”
Nilichogundua ni kwamba inahitajika
usafi na mpango wa kila siku kuifanya nyumba iwe nadhifu.
Soma hapa ugundue tabia hizi nane ambazo watu
wenye nyumba nadhifu wanazo, na huenda ukaamua kuziasili ili kukuwezesha kutoka
kwenye nyumba isiyo nadhifu ambayo umekuwa ukiishi:
1. Tandika Kitanda
Kabla hujaondoka
chumbani au nyumbani asubuhi hakikisha unatandika kitanda chako.
2.
Usiache vyombo vichafu jikoni
Kila wakati ambao jiko
halitumiki kusiwe na vyombo vichafu. Kufanya hivi kuweka jiko safi na pia
kunarahisisha maandalizi ya kupika chakula kingine.
3.
Weka utaratibu wa kufua nguo
Kuwa na utaratibu wa
kufua nguo chafu kunasaidia zisijilimbikize. Nguo chafu zinapokuwa nyingi ndani
ya nyumba kuleta muonekano wa mrundikano hasa kwa wale wenye familia kubwa.
4.
Tumia vikapu au vitenga kuweka mpangilio
Kunapokuwa na sehemu kwa kila kitu, ni rahisi kuweka kila kitu mahali
pake. Tumia vitenga na mashelfu kwenye kila chumba kwa ajili ya kuhifanyia vitu
vikubwa na vidogo.
5.
Fungua vitu vipya kutoka kwenye maboksi yake
Kitu kipya kinapoletwa
nyumbani kikiwa ndani ya boksi, kifungue ukiondoe kwenye boksi na ulitupe mara
moja.
6.
Usitupe nguo sakafuni
Hili ni jaribu kwa
wengi baada ya mihangaiko ya siku nzima jinsi gani wanahifadhi nguo walizokuwa wamevaa.
Kuendana na maisha ya siku nzima ya mhusika, nguo walizovaa siku hiyo watu
wenye nyumba nadhifu wana tabia ya kuzikunja, ama kuzitundika ama kuziweka
kwenye kapu la nguo za kufua badala ya kuzivua na kutupa sakafuni. Kufanya hivi
kutawezesha sakafu na nguo kwa pamoja vionekana safi.
7.
Safisha kadri unavyotumia
Unaweza kupunguza kiasi kikubwa cha uchafu kama utasafisha kadri
unavyotumia. Kama utasuuza ubao wa kukatia baada ya kuutumia wakati nyama
ikichemka au kuosha vyombo wakati wali ukiiva, vyombo vingi vitakuwa safi utakapofika
wakati wa kupakua chakula.
8.
Kamwe usiende kulala ukiacha jiko chafu
Kataa tabia ya
kukimbilia moja kwa moja kitandani baada
ya mlo wa usiku. Hakikisha unasafisha jiko lote usiku – osha
vyombo, futa kaunta na fagia sakafu mabaki yoyote ya chakula yaliyodondoka. Hi
pia itasaidia kutokaribisha panya na mende jikoni.
Kwa maoni au maswali
tembelea www.vivimachange.blogspot.com
No comments:
Post a Comment