1. Tandika kitanda.
2. Hifadhi documents
zote muhimu kwenye droo badala ya kuziacha zisambae kila mahali.
3. Tumia vizuri droo za
pembeni mwa kitanda kuhifadhia, hii itakusaidia sana.
4. Hifadhi hereni bangili
na vitupio sehemu moja maalum rahisi kuchukua na kutumia pale vinapohitajika.
Ni ahueni kujua kila kitu na sehemu yake.
5. Chumba kidogo cha kulala kinamaanisha
eneo finyu kwa kabati la nguo. Weka kitundikio rahisi . Pia ni pambo la chumba
chako ukipendacho.
7. Tumia ubao wa kutobolea
documents zinazotakiwa kutendewa kazi karibuni kama vile bill ndogondogo na pia
kumbukumbu za siku.
8. Tumia vizuri kona za
chumba. Mara nyingi huwa zinasahaulika. Unaweza kuweka vimeza kwenye kona na
vikakupa eneo zaidi la kuhifadhia vitu kama vitabu mapambo na picha.
9. Kama bado unafikiri
una vitu vingi basi tumia mvungu wa kitanda. Droo za mvunguni ni nzuri
kuhifadhia vitu kama shuka na mataulo.
10. Unakumbuka wakati
ilikuwa sawa kuweka picha ukutani kwa kutumia tape? Nyakati hizo zimeisha. Tumia
vitundikio maalum vya picha za ukutani na itasaidia kuondoa hali ya mrundikano.
No comments:
Post a Comment