Saturday, November 12, 2016

Namna ya kusafisha kochi la kitambaa

Makochi yanakuja kwenye malighafi mbalimbali za vitambaa pamoja na ngozi ila kwa hapa tunazungumzia yale makochi ya vitambaa. Vitambaa vingi vya makochi ni vigumu kusafishika kirahsi bila kuacha alama yoyote ya uchafu. Na wataalam wa kusafisha wanachaji gharama ambayo pengine huwezi kuimudu. Asante kwa uwepo wa dawa mbalimbali ambazo unaweza kutumia kusafishia kochi mwenyewe nyumbani.

Kwanza ili uweze kusafisha kochi la
kitambaa kwa usahihi unapaswa kujua aina ya kitambaa kilichotengenezea kochi hilo. Kusema kweli makochi mengi ya kutoka nje ya nchi yana maelezo ya aina ya kitambaa na njia ya kusafisha. Kwa mfano yapo yanayoweza kusema kuwa safisha na maji , na mengine ni kwa ukavu tuu (dry leaning). Ila kama umetengenezesha kochi hapa nyumbani inaweza kukupasa kuuliza aina ya kitambaa na utunzaji wake.  

Kwa aina yoyote ile ya usafishaji hakikisha unaanza kusafisha kochi kwa kuvua zile sehemu zinazovulika ili uzisafishie pembeni. Kwa mfano kama ni za kusafisha mwenyewe kwa maji na sabuni au ni kwa ajili ya kusafisha kwa dry cleaner.
Baada ya hapo brashi taka za juu  kama vile mchanga, udongo, manyoya ya wanyama wa kufugwa ndani, na mabaki ya chakula kwa kutumia brashi laini au mashine ya upepo.  Na vilevile sogeza mito ya kukalia na kusafisha eneo la chini ya mito hiyo kwakuwa taka nyingi zinadondokea na kujificha humo.

Kama kochi linahusika na kutumia dawa za kusafishia hakikisha unanunua iliyo sahihi inayosema kuwa inatumika kusafishia makochi. Zingatia yale maeneo yaliyo chafu zaidi kama vile panapumzikia kichwa na mikono kwani maeneo haya yanaweza kuhitaji umakini zaidi.

Kama kitambaa cha kochi kinaruhusu kutumia maji basi  kwa haya maeneo yaliyobaki ambayo hayavuliki tengeneza povu  na tumia brashi laini, kitambaa au sponji kuendana na kiwango cha uchafu na kuanza kusugua taratibu. Kumbuka huna haja ya kutumia maji mengi kiasi kwamba yanachuruzika sakafuni. Baada ya hapo chukua maji matupu bila sabuni na yakiwa ni ya uvuguvugu yatafaa zaidi, pamoja na taulo jeupe.
Loanisha taulo na anza kufuta kule ulikosugua na povu hadi taulo linyonye uchafu wote kiasi kwamba mzunguko wa mwisho hautaoinyesha uchafu wowote kwenye taulo. Uwe makini na kitambaa kinachochuja ukadhani ni uchafu kumbe sio. Baada ya kujiridhisha kuwa kochi ni safi kabisa basi ni wakati wa kuliacha likauke aidha kwa kulitoa nje au kwa kufungua madirisha kuruhusu upepo kuharakisha zoezi hilo.

Tukija kwa kochi lenye maelezo kuwa lisafishwe kwa dry cleaning tuu, maadam unakuwa umeshaondoa vile vitambaa vya eneo kubwa ambalo ni lile la kuvulika basi kinachofuata ni kutengeneza kiniminika cha usafishaji huo na anza kusafisha, baada ya hapo fanya lile zoezi la kufuta kwa taulo jeupe safi ili kuondoa hicho kimiminika ulichosafishia na pia kujiridhisha kwamba kochi limetakata kwa kutokuacha uchafu wowote ule kwenye taulo.

Zile foronya na vitambaa vingine 

ulizovua kusafishia pembeni vikiwa

tayari valisha upya na hakika unakuwa 

na kochi safi.

No comments:

Post a Comment