Hapa vikoi vimetupiwa kwenye sofa na coffee table, ila hapo kwenye meza kakikunja na kukitupia kwa mkato. Pia angalia jinsi rangi nyeupe ya vikoi ilivyochangamsha hilo sofa jeusi, kwahivyo moja kwa moja utaona kuwa unaweza kutumia vikoi kubadili rangi sebuleni bila gharama kubwa. Halafu ukiangalia zaidi pattern za vikoi zinaendana na za carpet.
Kikoi hapa kwenye meza kimetupiwa kizima bila kukunjwa lakini nusu ya meza na kimebaki kipande kinaning'inia
Hapa kikoi kimekunjwa na kutupiwa eneo la meza la kati tu
Licha ya vile kule kwenye sofa, hiki kikoi kizima bila kukunjwa kimetupiwa kwenye meza yote kikafunika kila mahali....kazi kwako mdau ideas hizoo cheza nazo upambe unapoishi..na ukimaliza naomba nirushie picha.
Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani ambayo unataka Watanzania waijue? Nijulishe simu/whatsapp 0755200023
Nimependa upambaji wako sijui nikupate wapi unifundishe.
ReplyDelete