Kuna aina nyingi za majiko ambazo wewe mdada unayeanza familia unaweza kuchagua kulifanya jiko lako kuwa na mashiko na kufanya kazi iliyokusudiwa kwenye nyumba. Siku hizi imekuwa rahisi kupata mawazo kwa kuchungulia dondoo mbalimbali kwenye majarida, kudesa la jirani au rafiki, kuangalia video na mitandao mbalimbali kwa mfano unavyosoma hapa sasa.
Muonekano wa jiko kwa asilimia kubwa unachukuliwa na tile na makabati. Tile za floor na ukuta wa jiko, zipo za kumwaga, ni wewe tu kuamua rangi na muundo upi unataka na kwa finishing ipi.
Kitu kingine unatakiwa kuzingatia kwenye design ya jiko ni makabati. Hard wood eg mkongo, mninga ndio mambo yote na ni muhimu sana, usidanganyike kwa urembo wa soft wood kwani si lolote si chochote kwa jikoni. Jiko litolee gharama lidumu.
No comments:
Post a Comment