Wednesday, April 13, 2016

Shughuli za kufanya kwenye bustani yako kipindi hiki cha masika



Mimea ya kwenye bustani ambayo ni pamoja na miti, maua na ukoka inahitaji maji kwahivyo majira haya ya mwaka kwa wapenda bustani ndio wakati sahihi wa kuiboresha. Ni wakati wa vifaa kama chepe, reki, mkasi, panga, mabuti na toroli kutolewa stoo kwenda kushughuli
kia bustani. Ni wakati wa kwenda kwenye bustani na kuanza kupunguza miti, maua na hata kukata majani. Ni wakati wa kuipendezesha bustani katika maeneo mbalimbali yanayohusiana na upatikanaji maji kwa wingi kwa kipindi chote hiki cha mvua. Na hata kwa wale waliopanga kuanzisha bustani huu ndio wakati muafaka.

Kipindi hiki ndio kinafaa kwa shughuli mbalimbali za bustani kama vile kuweka mbolea, kundoa mimea na maua makavu yaliyozeeka na magugu yanayoshambualia ukoka wako. Wakati huu ni mzuri kwani ardhi ina maji mengi ya mvua kwahivyo udongo ni mlaini kwa kung’oa visivyohitajika. Endapo unahitaji kuotesha  maua na mimea mipya, sasa ndio wakati wake. Mizizi itashika kwa kasi kutokana na mvua zinazonyesha. Ni wakati wa kuziba viraka kwenye maeneo ya ukoka ambayo yanahitaji kufanyiwa hivyo. Kama kuna mbegu za maua unazotaka kuanziashia vitalu na vitanda vya maua sasa ndio wakati wake.


Ukiweka mbolea kwenye ukoka na maua yako kipindi hiki cha mvua ni hakika kuwa utafaidi matokeo yake kwani maji ya mvua yanarahisisha kuizamisha chini kwenye mizizi.

Kwa upande wa bustani za kwenye vyungu vya sakafuni ni wakati wa kuotesha upya mimea jamii ya feni bila kusahau vile vya kuning’inia ambavyo vinahitaji kuondolewa maua yaliyoharibiwa na kiangazi na kuotesha mapya madogomadogo na hata waweza kuchanganya kadhaa ya aina tofauti kwenye chungu kimoja mithili ya kachumbari kwenye sahani, yanapendeza.

Wapo wenye maeneo ya kukaa kwenye bustani ambapo kuna kivuli lakini mvua ya upepo inaweza kuharibu viti na mito. Kama ndivyo kwa upande wako, basi yafaa kuviingiza vitu hivi stoo hadi pale mvua zitakapoisha.

Wakati huu ni wakati wa kusafisha na kuboresha maeneo mbalimbali ya kisanifu yaliyo nje ya nyumba yako.


Vivi anakuwezesha kupendezesha nyumba yako.  Simu 0755 200023

No comments:

Post a Comment