Tuesday, April 26, 2016

Faida za Mabafu ya Cubic



Kwa nyumba za kisasa za nyakati hizi, wenye nyumba wengi wanapenda kutumia mabafu ya cubic. Haya ni mabafu ambayo ni kichumba kidogo cha kuogea ambacho kinasimikwa ndani ya chumba cha bafu. Mengi ya mabafu haya ni ya kioo na mara yanaposimikwa yanaweza kudumu maisha yakie
ndelea kutumika bila tatizo. Yanapendwa kwenye nyumba nyingi zenye watu wadogo na wa makamo na hata wazee.

Zifuatazo ni faida zake:

Yanarahisisha usafi na utunzaji wa bafuni
Mara unapokuwa umesimika bafu lako la cubic kinachotakiwa ni kutumia na kusafisha ndani mwake ambapo ni eneo dogo sana  badala ya chumba kizima cha bafu. Hii imerahishiwa kwa ajili ndipo hapo tu panapogusana na maji wakati wa kuoga. Kwahivyo kazi ya kusafisha na kuweka bafu kavu ni ndogo ulishangisha na  mabafu yasiyokuwa na cubic hizi. Hii inamhakikishia mtumiaji wa bafu afya njema na usafi siku zote.

Yanachukua eneo dogo
Mabafu ya cubic ni madogo na kiukweli yanafiti karibia katika kila bafu. Unachohitaji tu ni kuta za kona kwa ajili ya kulisimika. Kwa makazi ya kisasa ya nyumba ndogondogo hasa maeneo ya mijini ambapo chumba kimoja cha bafu kinatumiwa na wanafamilia wengi, mabafu ya cubic ndio yanayofaa zaidi. Pia kwa Watanzania wengi ambao hawana uwezo wa mabafu makubwa au yale yenye sinki la kuogea ukiwa umekaa au umelala, lakini wanataka kuishi kwenye nyumba za kisasa, mabafu ya cubic yameonekana kuwa mkombozi mkubwa kwao.

Matumizi mazuri ya maji
Kama tujuavyo ni vyema kutumia vyema rasilimali ya maji. Kwa ajili mabafu ya cubic ni ya bomba la mvua matumizi yake ya maji ni kidogo kuliko bafu linguine lolole liwe ni lile la kubeba ndoo ya maji au la kujaza sinki la kuogea. Kwa bafu la cubic mtu mzima anaweza kuoga kwa nusu ndoo ya maji tu.

Urahisi wa matumizi
Ili kutenga eneo maalum la kuogea bafuni, kabla ya mabafu haya wengi waliweka pazia la bafuni. Endapo utakuwa na bafu la cubic huna haja ya pazia hilo tena.

Yanapendezesha bafu
Faida nyingine ya bafu za cubic ni kwamba zinakuja kwa miundo  na mitindo mbalimbali. Mabafu ya cubic yanachukua nafasi ya pambo la bafuni kutokana na kuta zake za vioo vya kuvutia.

Ni rahisi kusimika
Kusimika mabafu ya cubic haijalishi mpango wa awali wa chumba cha bafu husika. Hata sasa endapo una bafu la pazia ni rahisi kulibadilisha na kusimika la cubic. Au kama una la sinki la kuogea bado kuna kona ambayo unaweza kuongezea la cubic kwani halichukui nafasi kubwa na eneo la kuingilia na kutokea ni moja tu tena kwa mlango wa kuteleza.

Yanapatikana kwa bei tofauti
Yapo mabafu ya cubic yenye matumizi zaidi ya kuogea. Kwa mfano yapo ambayo mfumo wake wa umeme unawezesha kutekenya mwili au kutokwa jasho jingi (sauna). Unaweza kupata bafu la cubic kadri ya matumizi yako kwenye maduka ya vifaa vya bafuni.

Simu 0755 200023

No comments:

Post a Comment