Nguzo
za nyumba ni sehemu ya fahari ya usanifu wa nyumba ambapo zinaweza kuwa ni kwa
matumizi au ni kwa mapambo tu. Kuweka nguzo ndani na nje ya nyumba imekuwa ni
njia mojawapi ya kufanya muonekano wa nyumba uvutie zaidi. Katika historia ya
ujenzi, wahandisi na wasanifu wamekuwa wakibuni njia za kuongeza mvuto kwenye
majengo. Nguzo zimekuwa zikitumika kuleta muonekano wa kifahari ndani na nje ya
nyumba za kisasa na zinaweza kuwepo kwenye chumba chochote, japo zinapendeza
zaidi kwenye
vyumba vikubwa kama vile sebule na jiko la wazi.
Zaidi
ya kusaidia kubeba uzito wa nyumba hasa za ghorofa na kupeleka uzito sakafuni
nguzo zina maumbo maarufu mawili ambayo ni pembenne na duara. Na hata kama
zinakuwa na miferejji, reli au mabondemabonde lakini bado umbo kuu linabaki ni
mojawapo kati ya haya mawili. Sasa basi ili nguzo zivutie machoni inabidi
kuamua unazifunika na nini.
Zuberi Peter ambaye ni
mrembaji wa nguzo anatuambia kutegemea na mtindo wa ndani ya nyumba yako,
unatakiwa ufahamu ni urembo wa malighafi ipi ndio utafaa zaidi kwako. Kwamfano kama
ndani ya nyumba kuna muonekano wa kiutamaduni, nguzo zilizorembwa kwa urembo wa
kutengenezwa kwa saruji kali bila kuongezea mwingine ndio unaofaa zaidi.
Malighafi,
ukubwa na mitindo mbalimbali inatumika kuweka urembo kwenye nguzo. Malighafi
zinazotumika kwa nguzo za ndani ya nyumba ni pamoja na mawe ya asili ya granite, marble na mosaic. Malighafi nyingine
ni pamoja na plastiki, mbao, PVC, kioo cha nyuzi na chuma. PVC na plastiki ni urembo
wa bei rahisi lakini unaleta muonekano mzuri sana na wa kifahari. Mbao
zinatakiwa kwenye ngyuzo ambazo hazigusani na maji hata kidogo kwani zikishika
maji zinapinda. Chuma zinatumika kuzungushia nje ya urembo.
Nguzo za kwenye varanda
kwa ajili ziko mazingira ya nje zinapendeza zaidi zikirembwa kuendana na
maringira hayo. Mfano, inaweza kutengenezewa urembo wenye kuonekana kama
majani.
Kwa ushauri wa mapambo ya nyumba tuwasiliane 0755 200023
No comments:
Post a Comment