Friday, February 20, 2015

Chid Benz sasa akiri kosa mahakamani

Mwanamuziki Rashidi Abdallah Makwaro ‘Chid Benz’(29) amekiri mashtaka matatu yanayomabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kukutwa na dawa za kulevya, kifuu cha nazi na kijiko vinavyotumika kuvutia ama kunusa dawa hizo za kulevya.

Mwananchi linaripoti:

Chid Benz alikiri kufanya makosa hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema baada ya kuiomba Mahakama imsomee tena mashtaka yake hayo yanayomkabili.

Aliomba kusomewa mashtaka hayo yanayomkabili, muda mfupi baada ya kesi yake kutajwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Diana Lukendo kudai kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kuangalia kama utakuwa umekamilika ama la.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Chid Benz alinyoosha mkono na kuiomba Mmahakama imsomee tena mashtaka yanayomkabili, akasomewa na kukiri kuwa Oktoba 24,2014 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere alikamatwa akiwa na gramu 0.85 za dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye thamani ya Sh 38,638.

Pia, alikiri kukamatwa akiwa na vifaa vinavyounganishwa na matumizi ya kuvuta ama kunusa madawa hayo ya kulevya.

Baada ya kukiri mashtaka hayo yote matatu, Wakili wa Serikali , Lukendo aliiomba mahakama kutoa ahirisho fupi ili waweze kujiandaa na kumsomea maelezo ya makosa yanayomkabili. Hakimu Lema alikubaliana na ombi hilo na kuiahirisha kesi hadi Februari 23,2015.


Awali, Chid Benz aliposomewa mashtaka hayo yanayomkabili mahakamani hapo aliyakana yote na upande wa mashtaka ulieleza upelelezi wa kesi bado haujakamilika ikaendelea kuahirishwa hadi leo (jana) alipokiri makosa hayo.

No comments:

Post a Comment