Thursday, February 19, 2015

Fahamu jinsi akili ya mwanaume anayebaka inavyofanya kazi

Wanawake wa Uturuki sasa wameamua kuuvunja ukimya na kuzungumzia masuala ya ubakaji,unyanyasaji wa kinsia,na unyanyasaji kwa ujumla.BBC nchini Uturuki ilimuuliza Profesa maarufu nchini humo Sahika Yuksel, ni kwa namna gani akili ya mbakaji inavyofanya kazi.
Siku kadhaa zilizopita, ulimwengu ulishuhudia wanawake wa kila rika nchini Uturuki wakiandamana kutokana na tukio la ubakaji la msichana aliyekuwa na umri wa miaka ishirini aliyekuwa akisoma katika chuo kikuu nchini humo ambaye alibakwa na kisha kuuawa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Maandamano makuba yaliratibiwa na kusambaa kote nchini humo mwishoni mwa wiki wakitumia jina la binti aliyeuawa na lilitumika kwenye mitandao ya kijamii mara 3,300,000. Na zaidi ya hapo katika mitandao ya kijamii wanawake wengine pia waliibuka na majina ya wanawake waliohusika katika unyanyasaji wa kijinsia na kueleza kilichowakuta.

Kwanini wanaume wanabaka? Nini kinachosababisha ubakaji? Kwanini wanaume wanabaka?

Ni makosa makubwa kukisia kuwa wanaume wanabaka kutokana na matamanio ya miili yao. Mbona mwanamume aliyeko mtaani hawezi kumbaka mwanamke mpita njia kwa namna hiyo.pamoja na kutambua kwamba haifai,huthubutu kutekeleza ubakaji kwa usiri mkubwa ,mbali na macho ya watu.

Ubakaji si tendo la ndoa. Ubakaji ni shambulio, ni suala la nani mshindi, ni kama umeshikilia kitu na mwanamke ndiye mlengwa katika suala hili ni sula la mmoja mwenye nguvu ndiye anakuwa mshindi na wapo baadhi ya watu wanaopata faraja kutokana na ubakaji.

Ubakaji sio kosa pekee ambalo mwanaume huwa anafanya.Shambulio la mwili,mwili kudhuriwa ,kupuuzia haki za wanawake,na udhalilishaji ubakaji hutokea mara..
Raha hupotea ikiwa wewe utageuka kuwa muwindwa

Swali:je malezi ndiyo huzalisha mbakaji siku za usoni?

Watoto hukua katika mazingira ya kutakiwa kuwaheshimu wanaume na utamaduni wa kuonekana wanaume wana mamlaka zaidi ya jinsi ingine.mwanamke anatakiwa kumhudumia mumewe kwa namna tofauti zaidi na kutakiwa kutii mamlaka na utawala wa kimabavu wa mwanaume .

Na hapo ndipo mama husafirisha mtazamo na tabia hizo za kimfumo dume kwa watoto wa kike na wa kiume ,ni wazi kuwa mabinti wanaokulia katika familia zenye unyanyasaji wa kijinsia,hukumbana na unyanyasaji mkubwa zaidi katika ndoa zao ama katika mahusiano yao.

Wanaume walioshuhudia mama zao wakipigwa na baba zao wao pia huwa na tabia ya unyanyasaji katika mahusiano yao.wasicha na wavulana hutambulika katika jamii kwa namna mama zao walivyotendewa na baba zao na hiyo ndio sababu ya msingi.

Unaweza kusema kuwa hili ni tatizo la ulimwengu na unaweza kushuhudia matukio yenye sifa za kufanana ulimwenguni kote.lakini utofauti huonekana wakati wa kushughulikia ama kupambana na suala hili.wanawake nchini Uturuki huwa hawapati elimu ya kutosha kama ambavyo wanaume wanavyopewa kipamumbele.Nao wanasiasa wamemaliza mzizi wa fitna na kuweka ubaguzi bayana kwa kudai kuwa wanawake na waume hawawiani.
Ukinzani shurti utokee kwa tabia chafu

swali:Unawezaje kujihusisha na mwanaume mwenye mtazamo na tabia za namna hiyo na mhitaji?

Hakuna atakaye weza kuibadili kama hatang’amua na kukubali kuwa tabia zake ni mbaya na kuwajibika kwazo.kama atakamatwa na kukiri kuwa hakumaanisha kutenda hayo hii haitaleta mabadiliko ya tabia.

Idadi ya wanaume wanaogundua tabia zao zisizofaa zenye kuathiri jinsi ingine na kuhitaji msaada kabla hawakamatwa ni ndogo mno.

Namna pekee ya kukabiliana na tabia za namna hii ni kuwaweka katika vituo vya mabadiliko ya tabia wanaume wenye tabia za nman hii wakati wakitumikia vifungo vyao.Njia hii haitumiki sana nchini Uturuki .kila mmoja ana haki ya kuhudumiwa na kutafutiwa tiba ya tatizo lake.

Vipo vituo vingi vinavyoshughulika na mabadiliko ya tabia kwa wabakaji ulimwenguni ,na matukio ya kushambuliana wao kwa wao ni machache mno ukilinganisha na wale wasiopatiwa huduma hiyo jela.mpango huu wa tiba ni maalumu kwa vijana waliobalehe na wenye tabia za unyanyasaji wa jinsia .

Ningependa kugusia suala moja katika mazungumzo haya .Kuna haja ya kuwahasi wanaume wabakaji lakini nadhani adhabu ya kifo inahitajika tena.Lakini adhabu ya kifo si kibinadamu, sote tunajua ya kwamba nchini Marekani ,matukio ya uhalifu si ya kiwango cha chini katika nchi ambayo adhabu ya kifo inatekelezwa.

Hatua hii ya adhabu ya kifo sio kipimo tosha cha kukomesha uhalifu.watu walio katika nafasi za juu za uongozi hujaribu kutuliza jamii za watu.na mara zote maandamano na kelele hizi husikika mara tu matukio ya ubakaji yanapotukia,hatuzungumzii suala la ulipizaji wa kisasi hapa.lengo letu ni kwa jamii zetu kuwa huru na unyanyasaji wa kingono na ubakaji kadiri inavyowezekana.
Vunja ukimya.

swali: Mwanamke wa umri wowote aliyebakwa afanye nini,kama atakuwa jasiri wa kusema kuwa kabakwa.

Katika jamii na tamaduni zetu ambako suala la ngono limefanywa kuwa suala la kawaida na ndoa za utotoni ama za mapema naweza kusema zinapingwa, mashambulio ya kingono huwa ni nadra kutukia.

Mbakaji analijua hili fika lakini humtisha mwanamke anayembaka kuwa ataifahamisha familia ya mwanamke huyo kilichotokea na huendelea kutenda kosa hilo lililo kinyume cha utu.na wakati mwingine humgeuka mwanamke anaymbaka na kuwaeleza marafiki zake juu ya mwanamke huyo kwa matukio mengine zaidi ya ubakaji.

Mwanamke aliyebakwa anaweza kuchukua hatua za kisheria,anaweza pia kupata msaada wa kisaikolojia na uungwaji mkono na jamii. Lakini pia anaweza kuongea na marafiki zake wa karibu anaowaamini.Na hii ndio njia pekee ya kupata uponyaji ama nafuu ya matukio ya mashambulio ya kingono ama unyanyasaji na usikae kimya juu ya masuala ya namna hiyo.
jamii ikiwa pamoja huleta ahueni

Mashambulizi ya kingono yanaweza kuleta matatizo ya kiafya,magonjwa ya kuambukiza na hata ujauzito.zaidi ya hayo mwananke aliyebakwa anapaswa kuchunguzwa haraka iwezekanavyo na hatua za haraka hazina budi kuchukuliwa dhidi yake kiafya.

Inawezekana kukawa na matatizo ya muda mfupi ama ya muda mrefu ambayo yanahitaji huduma baada ya ubakaji kutokea.lakini pia kuna haja ya kuwa na vituo vya kuhudumia watu waliokumbana na unyanyasaji wa kijinsia,mahala ambapo msaada stahiki unapatikana na kutolewa mara moja bila kukawia.


Pia mwanamume ambaye mpenzi wake amekumbwa na unyanyasaji wa kijinsia hana budi kuwa na mpenziwe katika kipindi hicho kigumu na wakati huo huo akipokea matibabu ya kisaikolojia na msaada wa kijamii pia.

No comments:

Post a Comment