Sunday, February 15, 2015

KUTOKA KWANGU: Kwanini utandike kitanda?

Ni kama swali la kijinga vile, “kwanini nitandike kitanda?”
Sababu chache hizi hapa kwa kadri ninavyoona mimi:
Ni tabia nzuri ambayo ukijijengea itakujenga kwa tabia zingine nzuri zaidi, kutumia dakika mbili asubuhi kutandika kitanda chako ni tabia njema.

Kitanda kilichovurugika kinafanya chumba kizima kionekane mvurugano, wakati ambapo kitanda kilichotandikwa kinafanya chumba kionekane nadhifu hata kama vitu vingine haviko sawa kivile.

Nyumba zetu hizi tunavyozijua, si ajabu kukuta umelala na mdudu kitandani wakati kitanda 
kingekuwa kimetandikwa ingekuwa rahisi kumuona.

Kutandika kitanda inakupa morali wa kutoka kwenda kutafuta rizki badala ya kurudi kitandani kulala.

Unaburudika wakati unaporudi nyumbani na kuingia chumbani kitanda kikiwa kimetandikwa.

Inazuia aibu, nina uhakika huenda ulishakutana na hili, unaacha nyumba/chumba chako shaghalabagala mara unapata mgeni ambaye hukumtegemea. Hata ukisema aah, I don’t care…nina uhakika unajisikia aibu fulani hivi ndani ya nafsi.

Kwanini unaosha vyombo? Unaenda kuvitumia tena, sio? Kwanini unamwaga taka, kwani hutazalisha tena taka baadaye? Kufanya kitu kimoja kiwe katika hali ya usafi kinakupa hatua nyingine ya kusonga mbele. Hata kama huwezi kufanya chochote lakini hushindwi kutandika kitanda chako.

Kutandika kitanda haitakiwi kuwa ishu, ni kiasi cha kunyoosha shuka, panga mito na tandaza blanketi, basi.


Kwa mawazo yako ni nini faida na hasara za kutandika kitanda?

No comments:

Post a Comment