Saturday, February 28, 2015

----nitavukaje----Kutoka Sales Manager hadi Business Owner

Solar panel ikifungwa juu ya paa
Benard ni mmliki wa kampuni ya vifaa vya kufunga umeme wa jua kwenye majengo ya makazi na ya biashara. Anasema alichosomea yeye ni Environmental Science na alipotoka shule aliajiriwa kama sales manager kwenye kampuni iliyokuwa ikihusika na solar energy. Baada ya miaka sita akaamua kujiajiri.

Nimemuuliza kwanini aliamua kujiajiri. Akasema ni impact aliyoona kwa vifaa vya solar walivyokuwa wakifungia wateja wao. Kwa mfano kubadilisha dispensary ya kijijini iliyokuwa ikitumia kibatari na kufanikiwa kutumia taa, feni na computer walau moja. Kwake hiyo ilimgusa sana ndipo akasema naye anataka kuwa na kampuni yake ili aweze kuendelea kusaidia watu kwa namna hiyo hiyo kwa wingi na uhuru zaidi.

Benard anasema katika kujiajiri unapata kila unachokitaka kwa muda wako ila mwisho wa mwezi unatoa badala ya kupokea. Yani alipokuwa ameajiriwa yeye alichokuwa anajua ni kuwa mwisho wa mwezi anapokea, lakini kwa sasa kuwa na kampuni yake tofauti ni kuwa mwisho wa mwezi anatoa. Na hapo ndipo penye changamoto kubwa mno anasema. Ukiwa umejiajiri unaweza kulala, kusafiri, kufanya chochote unachotaka na kwa muda wako bila mtu kukupangia, ila kimbembe ni mwisho wa mwezi.

Benard anashauri ni vyema mtu anapotoka shule aajiriwe kwanza kabla ya kujiajiri. Kwanini? Kwa sababu anasema unapojiajiri una manage watu, sasa kama hukuwa mwenyewe managed inakuwa ngumu kujua ilivyo vigumu ku manage watu. Watu hawako so pefect kwahivyo wakubali walivyo, anasema.

Benard anasema pamoja na changamoto za hapa na pale anajivunia zaidi kujiajiri kuliko kuajiriwa, anafunga inveta za kuchaji kwa umeme na za kuchaji kwa solar, heater za solar za maji ya moto na solar za majumbani na maofsini. Kwa hivyo hizi inveta za kuchaji kwa umeme ni kwamba umeme unapokuwepo unachaji inveta yako, endapo utakatika unaiwasha, haina kelele na haihitaji system mpya ya waya, inatumia zilezile za umeme wa kawaida, kinachokuwepo ndani ni kiboksi kidogo tu.
inveta na betri yake
Bei ya hizi solar zina range kuanzia milioni moja na nusu hadi milioni 20. Kwa mfano anasema mfumo wa solar wa kuweza kuwasha laptop 1, TV 1 na taa 6 gharama yake ni milioni moja na laki nane.


Umehamasika? Usikose “nitavukaje” itakayofuata.

No comments:

Post a Comment