Thursday, February 19, 2015

Jinsi ya kutofautisha taulo za rangi moja endapo mnashirikiana bafu

Pale ambapo mtu zaidi ya mmoja anatumia bafu hilohilo, taulo zinakuwa ishu. Hapana shaka na wewe ulishakutana na hili. Unaingia bafuni unatoka kuoga unavuta taulo kujifuta, unagundua kuwa lina unyevu. 
Pasipo shaka hakuna anayependa kushirikiana taulo, sasa ugumu unakuja hasa pale taulo zinapokuwa za rangi moja.
Leo nakupa suluhisho rahisi sana unaweza hata kufanya mwenyewe: shonea kishikizo cha ribon ya rangi tofauti kwa kila taulo kwahivyo kila mtumiaji wa bafu hilo anakuwa na rangi yake.

 Tangaza rasmi rangi ya kila mwanafamilia (na pia rangi nyingine kwa wageni) na endelea kwa kujiamini.

Wakati mwingine utakapovuta taulo hutajikuta kwa bahati mbaya una share na mtu mwingine. Na faida zaidi ni kuwa badala ya fimbo ya taulo, pigilia hook kwenye ukuta wa bafu na tumia hizo ribon kutundikia kila taulo kivyake. Hakuna tena taulo zinazoanguka chini na hook pia zinasaidia ku save nafasi.

Ukiwa kama mama wa familia walio chini yako wanakutegemea uwaongoze kwa hivyo ni vyema kuwa na mbinu mbalimbali ili kufanya maisha hapo nyumbani yaende smooth..

No comments:

Post a Comment