Sunday, February 15, 2015

Utata sakata la mbunge aliyetelekeza mtoto

Unakumbuka nilishawahi kuandika hiki kisa tena hapa , kuna utata kwakweli, natumai weledi utatumika kufikia muafaka kati ya wazazi hawa wawili. 

Utata umezidi kugubika sakata la Mbunge wa Dimani Zanzibar, Abdallah Sheriya Ameir, anayedaiwa kutelekeza mtoto mwenye ulemavu mwenye umri wa miaka minne.
Licha ya mbunge huyo kudai kuwa amekuwa akimhudumia mwanaye lakini mtalaka wake, Hawa Aloyce, amedai mbunge huyo hajawahi kumhudumia mtoto huyo kwa lolote licha ya kuhitaji msaada kwa muda mrefu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ameir, alisema aliachana na mkewe Agosti 18, mwaka jana, na alimrudisha kwa wazazi wake wilayani Bunda na baada ya kikao cha familia walikubaliana kwa kuwa wameshindwa kuendelea kuishi pamoja mtoto abaki kwa bibi yake ( Mama mzazi wa Hawa).

"Sijatelekeza mke na mtoto bali nimeachana na mke na ninatunza mtoto wangu, tumeoana miaka tisa iliyopita na tumejaliwa watoto wanne mmoja alifariki, wawili naishi nao na ninawasomesha na kuwapa mahitaji yote muhimu, mmoja amemng'ang'ania, " alisema na kuongeza;

" Mwanangu ana Bima ya afya ambayo anatakiwa kutumia, anatakiwa kutibiwa na hospitali ya Agha Khan, lakini kwa makusudi mama yake hampeleki, badala yake anamtangaza kwenye vyombo vya habari kuwa anaumwa na amekosa fedha za matibabu anaomba Watanzania wamchangie, huo ni utapeli na Watanzania wasikubali kuingizwa kwenye utapeli kabisa," alisema.

Alisema ana ushahidi wa jinsi alivyokuwa akituma fedha za matumizi na utayari wake kuishi na kumlea mwanawe lakini Hawa amekataa na sasa anamtembeza mwanaye kama mradi maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam akiomba msaada.

Kaka wa mama yake Hawa, Jeremia Lameck, akizungumza na waandishi wa habari alisema alihusika katika shauri la kutengana kwa wanandoa hao na ushauri uliotolewa mbele ya watumishi wa idara ya ustawi wa jamii Bunda na kutakiwa mtoto abaki kwa bibi yake.

Kwa upande wake, Hawa alipoulizwa na NIPASHE kwa njia ya simu, juu ya madai hayo alisema mbunge huyo hataki kumtunza mtoto huyo na bima ya afya aliyoitoa ni mfu haikubaliki kwenye hospitali anakokwenda na kulazimika kutumia fedha.

"Hadi navyoongea na wewe hajawahi kuhudumia mtoto, alinifukuza kwenye nyumba yake, sijawahi kupewa kadi ya matibabu ya hospitali ya Agha Khan...kwa sasa nimefungua kesi Mahakama Kuu nikidai haki ya kugawana mali na kesi nyingine Mahakama ya Kisutu ya kudai matunzo ya mtoto," alisema.

Mama mzazi wa Hawa, Jennifer Kundami, alipoulizwa na NIPASHE kwa njia ya simu, alisema ugomvi wa ndoa haufahamu ila anaifahamu baada ya kikao cha familia iliamuliwa mtoto abaki kwake na Mbunge alikuwa anatuma fedha za matumizi.

Alisema askari na maafisa ustawi wa jamii walimsihi a muachie mtoto lakini alikataa na kudai anakwenda kupigania haki yake na kwamba mtoto siyo wake hawezi  kumng'ang'ania.

No comments:

Post a Comment