Friday, February 27, 2015

Kilimanjaro waongoza kwa kutelekeza familia

Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro, Leonidas Gama.
Jamani ya kweli haya? Wachaga tunaenda kuhangaika kutafuta masha na sio telekezo...

Mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa ukatili wa kijinsia wa utelekezaji familia kutokana na waume kufukuza wake zao na watoto na kuchangia ongezeko la watoto wa mitaani.
Akizungumza juzi na waandishi katika mafunzo yalioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), kuhusu uandikaji wa matukio ya ukatili wa kijinsia, Inspekta Msaidizi wa Polisi wa Dawati la Jinsia Mkoa huo, Priscal

Maganga, alisema wanaume mkoani humo wanaongoza kutelekeza familia zao bila ya kujali kuwa watakula na kulala wapi.
 
Priscal alisema katika kipindi cha  Januari hadi Februari mwaka huu, wamepokea kesi 20 za waume kutekeleza familia.
 
“Mbaya zaidi unakuta mama na watoto wanafukuzwa usiku wa manane, hawajala, hawana pa kukimbilia wanakuja hapa kwetu wakiamini tutawapa chakula na maradhi  na sisi Polisi hatuna fungu hilo, inatubidi tuingie mfukoni kuchangishana ili kuwasaidia,”alisema.
 
Hata hivyo alisema kesi hizo zimepungua kutoka  kesi 50 walizokuwa wakipokea kwa mwezi kutokana na elimu wanayotoa kwenye mikusanyiko ya watu.
 
Alisema kupungua kwa kesi hiyo kunatokana na elimu wanayotoa kwenye mikusanyiko ya watu ya madhara ya kutelekeza familia.
 
Priscal alisema kwa upande wa ukatili wa kubaka, wamepokea kesi tano katika kipindi hicho, tatu za kulawiti na moja ya ukatili dhidi ya mtoto aliyepigwa na wazazi wake kupita kiasi.
 

“Kesi hizi za kulawiti na kubaka nyingi zipo shuleni na hasa Manispaa ya Moshi," alisema na kusisitiza kuwa: " Kunahitajika wazazi kushirikiana na walimu na dawati kutoa elimu kwa watoto wao kuwaeleza madhara ya ukatili huo." 
Chanzo: Nipashe

No comments:

Post a Comment